Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Ni makosa kufikiria muda unakwenda.
Muda hauendi. Muda upo mpaka utimilifu wa dahari
Wewe ndiye unayeenda.
Huupotezi muda. Muda hauna mwisho. Unajipoteza mwenyewe.maana una mwisho wako
Ni wewe unazeeka na kufa. Muda haufi. Kwa hivyo jitumie vyema kabla ya muda wako kuisha.
Na mojawapo ya mambo mabaya zaidi ya kufanya na wakati ni kujilinganisha na wengine.
Ng'ombe hula nyasi na kunenepa lakini mbwa akila majani atakufa. Kamwe usijilinganishe na wengine. Ishi maisha yako
Kinachofaa kwa mtu mwingine kinaweza kuwa ndicho kitakachokuua. Zingatia karama na talanta ambazo Mungu alikupa na usiwe na wivu kwa baraka alizowapa wengine...
Wote Simba na papa ni wawindaji wa kitaalamu na ni wawindaji hodari, lakini
Simba hawezi kuwinda Baharini na Papa hawezi kuwinda msituni...
Kwamba Simba hawezi kuwinda baharini haimfanyi kuwa mnyama asiyefaa Kwa uwindaji na kwamba papa hawezi kuwinda msituni pia haimfanyi kuwa mnyama kwa uwindaji asiyefaa... wote wawili wana eneo lao ambapo wanaweza kufanya vizuri.
Pamoja na kuwa UA rose lina harufu nzuri zaidi kuliko nyanya, haimaanishi kuwa inaweza kufaa kutengeneza mboga...
Usijaribu kujilinganisha na wengine.
Wewe pia una nguvu zako mwenyewe, jitafute na ujenge juu ya nguvu zako na uwezo wako mwenyewe
Wanyama wote waliopo leo.. Kwa mujibu wa maandiko matakatifu walikuwa ndani ya safina ya Nuhu. Konokono ni mmoja wa wanyama hao. Ikiwa Mungu aliweza kusubiri kwa muda wa kutosha kwa konokono kuingia katika safina ya Nuhu; Mlango wake wa neema hautafungwa kwako hadi ufikie nafasi unayotarajia maishani.
Usijidharau kamwe, endelea kutarajia baraka zako.. Maana haziko mbali sasa.. Na huu ni wakati wako wa kutabasamu tena!
Kumbuka kwamba Mungu hawahi wala hachelewi bali hujibu maombi yote kwa wakati sahihi huwezi kamwe kujua jinsi ulivyo karibu na lengo lako.
Heri ya mwaka mpya wewe utakayebarikiwa kusoma uzi huu..
NAKUOMBEA
Mshana Jr
Future pastor❤