Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Unajitahidi kueleza usivyo vijua, the bottom line is hakuna mtu yeyote yule mwenye haki au miliki dhidi ya mtu mwingine kwamba unaweza amka tu ukajisikia kufanya chochote eti kisa ni mtoto , na pia huwez niambia au nifundisha kuhusu maisha magumu au kutokua na mzazi/wazazi , nimepita huko , huwez piga mtu mzima eti kisa n mzazi , nakunyoosha

Nilichokuzidi hapo ni ufahamu, hizo nadharia baki nazo
 
Asante sana Kiongozi. Ushauri umenifikia vyema
 
pole sana mkuu usichoke kutafuta amani ipo siku utaipata,. Muombe sana Mungu akupe hekima na akufungulie njia hakuna linaloshindikana
 
Naomba nijibu swali UNAMUAMINI MTU YEYOTE AU??

Kuamini watu wa karibu ishanitia hasara sanaa
Ukisema usimwamini mtu yeyote ni sawa kusema pia unachosema nisikiamini. Sasa sijui utakuwa mtu wa aina gani! Inabidi angalau uuamini watu fulani, hata kama kuna waliokufanyia mabaya maana si watu wote waliokufanyia hivyo. Amini wazazi wako, ndugu zako wanaoweza kuaminika, rafiki, colleagues, jirani etc. Mimi namwamini mtu hata kama nimekutana naye siku hiyo kwa kutegemea ninavyojisikia moyoni: kama moyo haushtuki, huyo mtu nitamwamini, na moyo ukishtuka nita'suspend' kumwamini kwa muda mpaka nipate uhakika zaidi.
 
Hujawahi kupigwa tukio mkuu ngoja waje wakupige tukio
 
Unaweza vipi kumtwanga kofi mamaako au kumpiga babaako hautafanikiwa kwa lolote na ukifa ni motoni fanya ufanyavyo usuluhishwe hili kabla ujakata moto
Unaweza ukawa sawa na usiwe sawa kwa namna nyingine. Sina hakika kama Mungu hufanya Judgements zake kama binadamu tuwazavyo.

Binafsi Mungu kuniponya na kunitoa kwenye hali ya dhiki niliyokua nayo. Hata sasa ananilisha, ananivisha na naona nikipiga hatua kuelekea Nuru. pasina shaka hakutizama kosa langu lakini alitizima nafasi yangu.

Kufanikiwa au kutofanikiwa ni kudra za Mungu, Lakini angeangalia Unyofu wa Moyo ndo tufanikiwe basi hakuna Mwanadamu Mnyofu wote tuna mapungufu.

Labda Niku challenge kidogo. Kuna Wauaji, Wabakaji na Majambazi Duniani. Patia Picha wewe ni mtoto wa Hawa waovu, kwaio ukienda nao tofauti , et Mungu akufungie mafanikio kisa kikiwa umepingana na Wazazi wako?.
 
Bila baraka za wazazi hutamwona Mwenyewezi Mungu amini nakwambia lakini Rehema zake hazina mipaka utazipata zote na kusaza kwa hapa duniani
 
Kama ulio eleza ni ya kwel ,na umeshaomba msamaha ila hawataki basi kwanza jisamehe ww mwenyew,uamni kabsa kua Mungu alikusamehe ,na uendele na maisha
 
wewe unasumbuliwa na kiburi
wewe biashara ya kuuza bangi ndio inayokufaa kijana kama wewe hata ujumbe wa serikali ya mtaa huwezi pendekezwa,Baki na kiburi chako.
 
Mkuu kwenye kutafuta amani na wazazi wako zingatia sana kutunza amani ya moyo wako.Usijishushe uonekana kama takataka.
Unapotuma watu wao wanaona kuwa huwezi kuishi bila wao.Achana nao dili na familia utakayoianzisha.
Futa namba zao za simu,acha kuuliza habari zao,chukulia kama wamekufa.
Usiwe mnyonge kwenye maisha yako hayo mafupi.
 
Hujawahi kupigwa tukio mkuu ngoja waje wakupige tukio
Usiseme hivyo. Hata mimi nimepitia katika hali ya kumwamini mtu, lakini uaminifu wangu ukaniponza. Kwangu hali kama hiyo haina maana kwamba basi kuanzia Leo watu wote hawaaminiki, hapana. Kutakuwa na watu wanaoaminika na wengine hawataaminika - lakini si jambo sahihi kuwaweka watu wote katika kapu moja. Hata msemo "samaki mmoja akioza wote wameoza" haufanyi kazi kwa namna hiyo, maana si kweli kwamba samaki mmoja akioza, then wote wanakuwa wameoza. Sisi wavuvi msemo huu hauna maana hiyo.
 
Mkuu FORTUNE JR zingatia ushauri wangu. Mimi nimeshakutana na situation kama yako. Kama una amani moyoni na umeshajaribu kutafuta amani na Wazazi wako na wao hawakuelewi endelea na mambo yako. Wao wenyewe watakutafuta tu. Zingatia Wazazi nao ni binadamu kama wewe Mtoto. Kwanini Mungu aliruhusu yote hayo yakutokee? Na kila siku huja na mambo yake.
Zingatia maisha yako na uwajali na kuwathamini watu wote.
Wazazi wa Kiafrika ni jau sana Mkuu. Wanapenda kuheshimiwa na kuthamimiwa lakini wao hawapendi na hawataki kuiona hiyo thamani kwa kuwatendea mema Watoto wao.
 
💯
 
Pole sana.
Ila kumbuka "TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…