Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Kiukweli mimi si mtu wa kusapoti kupigana.
Ila we uchune bana weee endelea na maisha yako hao wazee wako ni kichomi.
Unapigaje mtoto uchi mbele ya watoto wenzie au majirani?
Hapa Marekani yangekuwa mengine kabisa.
 
Imefanya juhudi za kutosha kuwaomba msamaha lakini wao wamekaidi.

Umewatuma Hadi wazee Bado wamekaidi.

Umetuma Hadi pesa lakini pesa zinarudishwa na wamekaidi.

Ndugu yangu laana huwa haiji kirahisi hivyo, RELAX endelea na maisha yako.


Kaa kimya Mungu atawapa pigo Takatifu Hadi watakuja kukumbuka wewe.

Kwenye Hilo sikulaumu. Upo sahihi hatua ulizozichukua za kuwaomba radhi.

Ila wao ndo tatizo.

Mungu tunamkosea mara ngapi? Ingekuwa Mungu nae hasamehi wote tungekuwa ARDHINI.

ACHANA NAO.KAA KIMYA WALA USITAKE KUJUA HABARI ZAO. MUNGU ATAWAONESHA
 
Wanaume hawajazoea kuoneshwa ukarimu, ukiwaonesha ukarimu wanadhani unawataka.

Ni vizuri kuchambua/kuelewa hisia za wanawake before kujiingiza mzima mzima.
Achana na mambo ya kuelewa hisia, huyo dem ana boyfriend wake ambae alimsaidia mwamba, leo tena anataka kumkula binti kisa anamuonesha wema.

Ni tamaa tu hamna kingine.
 
Mila zenu zipi??
Huyo dada na mleta uzi wana mila sawa??
Dada kwao wana kibunda, jamaa choka mbaya. Jinsi ya kuishi ni tofauti kabisa, wengine kiss la paji la uso ni kitu cha kawaida...

Shida ni kua jamaa anamtamani huyo binti, amefanyiwa wema kama rafiki yeye anahisi ni kwakua kapendwa.

Kumbuka pia huyu kijana hajawahi kufeel kuthaminiwa, so anahisi akifanyiwa kitu chema basi alimemfanyia ana sababu na sio unconditionally, watu wema wapo.
 
Ni mzazi mpumbavu anapiga makofi kijana aliyehitimu chuo kikuu. Kuna wazazi wangapi wameua watoto wao kipumbavu kwa kuwapiga? Mimi sioni kosa lolote la huyu kijana.
 
Endelea na maisha Yako.

Kama jitihada na bidii za kutafuta suluhu ulishazifanya sana.

Wale ni watu wazima Wana akili ila wamekosa HEKIMA na BUSARA hata kama ni wakubwa kwako.

Ukilazimisha sana kupewa msamaha litakalokukuta ni Halali Yako.

Anzisha Familia Yako na wewe Ili uwe bize na familia Yako.
 
Wandikie barua kueleza hisia Zako kwao, waombe msamaha wa kutoka moyoni kabisa.
 
HUYO MALAIKA KAKUOKOA TOKA KWENYE SHIMO LA KIFO BADO UNAWAZIA KUPATANA NA WALIOTAKA UANGAMIE(KWA MAELEZO YAKO KAMA HUJADANGANYA) PIGA CHINI FANYA MAENDELEO. HUWEZI JUA UKIPATANA NAO UTAKUTANA NA MAKUBWA YAPI TENA. KIFUPI WAZAZI WAKO SIO WEMA NA WALIKUWA WANAKUTAFUTIA POINT YA KUKUANGAMIZA USIFIKIRI HILO TUKIO LILIKUWA LA BAHATI MBAYA LILIPANGWA NA WAZAZI WAKO WOTE WAWILI. SIKU UTAKOYOJUA KUWA WAZAZI WAKO NI MAADUI ZAKO WAKUBWA HAPA DUNIANI UTAKUWA UMECHELEWA.
 
Pole sana mleta mada kwa mkasa uliopitia, kwa kiasi fulani kwa tamaduni na kawaida ya kwetu ulikosea kumrudishia mama na kumrudishia baba kile walicho kufanyia .
Kawaida yetu sisi binadamu tuna kisasi kisicho Isha mpaka tuone wale waliotufanyia baya wamepatwa na mabaya zaidi na zaidi, furaha yetu inakuwa kubwa pake wabaya wetu wanavyo pata magumu mengi.
Na ndivyo kwa wazazi wako, hawako na furaha kukuona ukonna angalao, pengii tamanio lao kukuona kwenye ubaya na magumu mengi na pengine hata usiwepo duniani.

Kwa vile moyo wako unekuwa radhi nao, ila wao hawajawa radhi nawe , wewe waache na kilicho chao, elekea mwelekeo mwingine, tembelea wagonjwa , wafungwa, wazee, wajane yatima na wote wenye mahitaji maalumu, toa kwao chochote ulicho jaliwa, toa kwa dhamira kama ungekuwa unawapa wazazi wako , toa elekeza baraka na matokeo mema ya matelo hayo kwa wazazi wako, wakati fulani wao wazazi ndio watakao kuja kutaka radhi nawe.

Huyo binti kwa ishara ulizosema kuna kitu kinamsukuma, kumbuka ni nadra sana mwanamke kufanya hisani yoyote kwa mwanaume asie na maslahi nae, kuna jinsi anakuchukulia ila anashindwa kuiwasilisha kwako, kumbuka ilvyokuwa si vizito kwake kukupa namba yakez kumbuka pia alivyo kuwa mwepesi kukusaidia kwa jinsi ulivyo eleza, kuna namna anakupenda ila hana namna ya kuonyesha kulingana na mazingira yaliyopo.

Cha kuganya acha muda uongee, kama ni wako hata iweje atakuwa wako na wewe kama ni wake ata iweje utakuwa wake.

Jitahidi mno usinyeshe kwake unampenzi, jitahidi sana, pia jitahidi usiwe na mpenzi, itakusaidia wakati yeye akitafuta mazingira rafiki.

Yote ya yote mwenyezi Mungu awe nawe awe pia na huyo dada, jitahidi kuhifay sana hela na kuiwekeza , jitahidi kutoa sadaka, epuka wanawake na mapenzi kwa ujumla, endela kutafuta masuluhisho na wazazi , onyesha shukrani na kujali kwa huyo dada lakini hakikisha unasimama kama mwanauy na unatumia akili yote ya kiume.

Iwe heri kwako ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…