Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Asante sana Kiongozi kwa Time yako. Ushauri umenifikia.
 
Bado hujaomba msamaha au kutaka suluhisho kwa kumaanisha,na wazazi wako wanafeel hivyo, nenda nyumbani hapo ulipofukuzwa, kawaangukie wazazi, watakufukuza usiondoke, endelea kulia nao, wataona kweli umemaanisha na watakusamehe. Na pia kama kweli unataka msamaha, msamehe mama yako toka moyoni kwa yale alokufabyia ukiwa mdogo, chukulia kwamba alikuwa na changamoto pia labda za kiakili kiasi cha kuwa mkatili kwako kiasi hicho. FANYA HIVYO KWA AJILI YAKO NA FAMILIA YAKO IJAYO(WATOTO).
 
Binti apelekewe moto, kwani hajielewi hadi a-play role part of wife materials kwa Kaka yake wa hiyari? Pia nani ana uhakika huyo Boyfriend wake atafikia hatua ya kuwa Mumewe, au wote waliokuwa wachumba walifanikiwa kufunga ndoa na kuishi pamoja?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Mzungu aliiweza ngozi nyeusi kwa kuleta dini na imani hata kwenye mambo ya kawaida
Angalau wewe umechangia kwa uhalisia sio hisia
Wazazi ni watu kama watu wengine, wanaweza kuwa ni wachawi,wezi,waongo na waovu kama waovu wengine kwenye jamii
Wakati mwingine Mungu anatutoa kutoka kwenye koo za kiovu lakini tunajifanya kung'ang'aniana.
Kuna mzee mmoja aliwahi niambia kama utani "zamani Wazazi walikuwa wanatoa laana lakini sio laana bali walikuwa wanakuroga ili kulinda heshima yao"
Mtoa mada anaweza akawa anamkimbilia Simba bila kujua
 
Kuna kitu nakifikiria, sina hakika nacho. Naomba kujua wazazi wako wamezaa watoto wangapi? Yaani una ndugu wangapi kutoka viunoni mwao? I want to connect some dots here. Kama ninacho kifikiria kitakua sahihi then nitakujibu inbox na sio hadharani
 
Ngoja nikuite MAN!

Usije kujilaumu Kwa lolote hasta kidogo!

Hicho ulichofanya ndio matunda wazazi wako wameyapanda kwako na wamevuna mavuno mema!!

Kama umewaomba msamaha umetimiza wajibu wa mtoto Kwa wazazi!!

Endelea na maisha Yako huku ukifuatilia maisha ya nyumbani kwenu wanaendeleaje!

Kama unataka kuwasaidia wasaidie kupitia ndugu zako was pembeni Kwa siri Ili wao wapate credit ya msaada huo nyuma ya pazia upon wewe!!

Huyo dada usitongoze japo sio mbaya akijua unampenda sana,lakini unamheshimu mchumba wake kwahio huwezi Fanya lolote lile !

Mungu yupo kabisa na alinisaidia sana,japo Kuna mambo Huwa yanakera sana anayotupitisha kwenye maisha mfano vipigo vya mbwa mwizi toka Kwa wazazi plus kutelekezwa utotoni plus wakati mwingine Mungu anatuletea wenzi was ajabu wenye roho mbaya kwenye maisha tena za kutisha sana!!

Lakini anabaki kuwa Mungu!!hivyo hivyo!
 
Sasa shida nini hayo maisha ya wazungu kitambo huna kosa mkuu wazazi wako wanaonekana wana shida sana ila familia nyingi za Africa ndio zipo hvyo.

Paul pogba hapatani na familia yake.
Mwakinyo hapatani na familia yke hivyo move on mkuu familia nyingi za Africa zipo hivyo ndugu na wazazi tunaona ni miungu watu.
 
Asante kwa stories nzuri mkuu,, je, umejaribu kumkumbuka yule Jamaa aliyekupokea mjini!? Maana kama siyo yeye usingekuwa hapo ulipo
 

Mimi na mzee hatuna mawasiliano mazuri sababu ya mambo yake wakati nakua, yananichoma moyo sana kila nikikumbuka

1. Nina alama za fimbo na viboko kwenye mwili wangu, alikua ananichapa na waya za umeme (unazichuna unabakiza zile za ndani) kila nikioga nikiziona nabaki kuumia tu

2. Alikua na maneno makali sana SANA SANA, si mbele ya watu au hadhira yeye anasema tu, Unasikia

a) "...yaani huyu bora ufuge mbwa atafukuza mwizi kuliko huyu.."

b)".. huyu huwezi kumwacha hata na nyumba ukakuta kitu kimefanyika.." ila mimi ndio nilikua punda wa nyumbani

c)"..yaani wewe hata huko kusoma sijui kama una akili ya kufaulu, tutatona hiyo form 4.." hii siku nilishindwa kuvumili nikabeba vyangu kuondoka nyumbani,Japo maza alinirudisha na hatukuwa tunaongea na mzee zaidi ya salamu tu, toka siku hii ndio nilipoteza hamu na huyu mzee, na form 4 nikafaulu.

Huwa simpigii simu hata miezi 6, mpaka apige yeye na huwa sina story nae, ni za huko wazima imeisha hiyo, anaelewa yoote haya sasa anashindwa kuniface maana huwa anasubiri naongea na maza nasema msalimie mzee Imeisha, ndio utasikia baba yako yupo hapa.

MZEE aliniHARASI sana aisee, nina makovu ndani ya moyo.

Tupo wa kiume 2, wote ni boti moja, na msichana m1 ndio ameiva nae

Nimepanga siku tuongee familia nzima, tuambizane ukweli wa maisha akielewa tutapatana na kuishi vema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…