Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Maneno ya Hekima na Busara umempa na kwa Faida ya wengi!
 
Wazazi nao pia ni binadamu wana personality tofauti tofauti kuna muda wanakosea ingawa hawawezi kukubali kosa, cha kufanya wewe jishushe omba msamaha na mara kwa mara wajulie hali tuma text hata wasipo jibu we tuma ukiwa na deal ukapata kiasi kidogo watumie na omba mungu arahisishe nyoyo zao na jipe muda mambo yatakuwa sawa
 
Pole sana Mkuu

Visa kwenye simulizi yako vinaonesha Kuna tatizo kwenye familia yenu, huenda ni stress za maisha ama ni asili ya familia yenu.

Huwezi kumpiga mtoto wa wastani wa miaka 24 hata kama amekukosea badala ya kumuelewesha taratibu.

Ulizia Kwa watu kama wewe ni mtoto halisi Kwa Wazazi wako, huenda walikurithi baada ya Wazazi wako halisi kufariki ama vinginevyo..
 
Endelea kumwomba Mungu hakuna jambo gumu kwake ipo siku utaelewana na wazazi wako
 
Kosa kubwa kumpiga mzazi,ni Bora umpotezee kuliko kunyanyua mkono kumpiga mzazi Kwa umri ulo kuwa nao,hakika ulipaswa kutokomea sehemu yoyote iwayo na kuwapotezea kuliko ulichokifanya.

Hili jambo litakuandama sana kichwani mwako daima dawamu na Kuna uwezekano wa kujirudia katika uzao wako.

Fanya kwenda kuomba msamaha Kwa wazazi wako Kwa gharama yoyote iwayo ili upate msamaha wa wazazi wako wangali hai.
 
Sasa mama ni mpiganaji na baba ni ngumi mkononi walitegemea wazae mtoto wa namna gani Kama sio Matumla ?

Ni hapo uliamua kuwacharaza kidogo ,🤣🤣 Anyway naweza kukushauri kuwa kwa umri wao wa chuo kipindi hiko haikuwa sahihi mama kukupiga ,lakini pia baba yako hakuwa sahihi kuingilia ugomvi kwa kuongozwa na hisia za mapenzi ,ila zaidi ulitumia hisia za hasira kuwapiga wazazi hivyo naweza kusema kuwa ninyi wote mlikosea na kwakuwa ulishaonesha juhudi za kuomba msamaha hawajajaribu kuonesha kukuelewa nakushauri endelea na maisha yako ikiwa wewe ulilitambua kosa lako ila wao bado hawajatambua makosa yao hivyo ipo siku wataelewa kuwa walianza wao kukukosea wewe hivyo na wewe ukajikuta na hasira tayari.
 
tumia vingozi wa dini kama wzazi ni waumini
hakuna mtu anabishia viongozi wa dini
ndugu ni wanafiki
 
Kama ulivyoomba Mungu akakusaidia endelea kuomba Mungu vivyo hivyo ipo siku utapata muafaka Mungu ni mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…