Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Naomba no, ya malaika kwanza kuna kitu ni muilizie maana naona kabisa kuna kitu sielewi elewi hivi.
 
Wazee wako inaonekana ni wenye hasira na vinyongo sana. Kitendo cha wao kukufukuza na wewe kuondoka kina maana uliwadharau. Rudi ukawaombe wakusamehe na sio kutumia watu.
Wazazi wako ni watu wanaoamini mtoto kwa mzazi hakui. Haitashangaza hata utakaporudi wakakunasa vibao tena. Watakufukuza, lakini simama katika kuwaonesha nia ya wewe kujishusha kwao.
 
Dah!....umepitia mengi mkuu, pole Sana...ila endelea kufanya juhudi huenda kuna siku mtapatana na wazazi wako usiwakatie tamaa.
 
Pole sana.
Inaonesha hauna ndugu wa tumbo moja. Hii inanipa taswira tofauti juu ya uhusiano wako na wazazi. Pengine (utaniwia radhi) walikuasili kutokana na wao kutokuweza kupata mtoto (jaribu kuchunguza).

Yote kwa yote, jitahidi kuwatendea wema wazazi wako hata ikiwa hawataki.
 
Tafuta mtu mmoja anaeheshimiana Sana na babako,nenda nae kwa wazazi wako, ukifika chakwanza anguka miguuni pa babako muombe msamaha akikubali ndipo mkae chini msalimiane akigoma ondoka ufanye patanisho na mungu wako kwa ajili ya kizazi chako Mungu Ni muaminifu Sana.
Hata maandiko yanasisitiza samehe 7*70 vile vile Kuna mahali pameandikwa ndugu akikukosea uite watu wawili watatu ufanye patanisho akikataa unawe mikono.
 
Wazazi wako huwenda walikua na shida ya akili ๐Ÿค”
Na yawezekana bado wanayo kama wanazidi kumkazia baada ya yeye kuambuwa kosa na kunia kuomba msamaha.
- kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, kwangu mie hii si kweli, kuna nyakati ambazo mmoja/ wachache wanaweza kuwa sahihi na wengi wakapotoka(reff. Galileo galilei na dunia kuzunguka jua?)
  • Asiombe kwa huyo binti anayemsaidia.
  • Wazazi wasaidie bila wao kujuwa,kupitia kwa ndugu unayemwamini. (Saidia kadiri ya uwezo wako usijikamuwe).
-Awe na amani moyoni kwani pamoja na kukaziwa na Wazazi yeye kafunguwa moyo wake yu tayari kuomba na kupokea msamaha,.....
 
Wewe ni mwenyeji wa wapi kiasili. Yaani ni kabila gani? Maana kama ni wachagga ningekupa akili ya kumaliza hiyo mambo. Kuna majani ukishikilia ukachanganya na asali na maziwa na damu na kondoo akatangulia na wazee wawili na mchungaji wasipokubali imekula kwao. Ila kama ni makabila mengine unaweza kutumia viongoz wa dini mkubwa kama askofu kama ni mkristo. Kama muislam vivyo hivyo. Wakikataa unaenda kutoa sadaka kanisani na wewe unaendelea na life lako. Mpaka pale amani ya Mungu itakapoamua mioyoni mwao watakutafuta. Japo hujatuambia kama una ndugu wakubwa au wadogo.
 
Watanzania tuna tabia ya kutokupenda kupima afya zetu , lazima tatizo la akili liwe kwa kiwango cha juu ndani ya jamaii, ndio maana unakutana na visa vya kustaajabisha kabisa ,mara Kabaka bibi wa miaka 100 ,Mara kabaka mbuzi shida ni hiyo.

Hata humu jf hilo tatizo lipo unakuta mtu badala akosoe mada anaanza kumwagia mtoa mada matusi ya nguoni๐Ÿค—
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ