Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Na wewe bwana kwani huyu kijana aliwaomba wamzae... Kigezo cha kuhudumiwa Hadi akue na kusomeshwa ilikuww wajibu wao. Msitumie kigezo cha kuwazaa watoto kuwatesa watoto kisaikolojia na kimwili.
Wote. Wamekoseana Ila walianza wao. Na bado amewaomba msamaha hawataki. Aache upepo upite aendelee na mishe zake
 
Naweza nikasema wazazi wako watakuwa na ugonjwa wa afya ya akili kipigo ulichokua unapewa si cha kawaida kabisa mtu mzima miaka 24 bado unatandikwa kama mtoto hii hapana wazazi wako wanaelekea kuugua ukichaa kabisa, wewe kikubwa pambana na maisha yako mwombe mungu akupe uzima na nguvu kama jitihada tayari umeshafanya kuwaomba radhi wazazi lakn bado wameweka ngumu iyo haikuzuii kuendelea na maisha yako, kwa upande wa uyo dada chonde chonde usije kumuonesha hisia za mapenzi utakuja kuharibu urafiki wenu kumbuka ulikotoka na upo wapi na unaelekea wapi.
 
Pol
Pole sana kwa hatua ya makuzi uliyopitia ni ngumu kidogo kuelewa hiyo kupigwa na kukalipiwa na mama yako kwa kila mara ulikuwa unafanyiwa wewe peke yako au na nduguzo kama wapo, pia nyakati zote hizo za kichapo toka kwa mama mzee alikuwa wapi? au alikuwa anachukua hatua gani kwa kuyaona hayo aliyokuwa anakutendea mama yako?. Nionavyo mimi mother hakuwa anakutendea haki na mzee pia akawa anapotezea so kama ulivyosema mother ni mtu wa hasira na kisilani so wewe ndio ulikuwa mnyonge wake wa kumalizia hasira zake (Purching Bag) ikakufanya wewe kukua na hiyo hali ya kuwa hupendwi na wazazi wako hasa mother. Thats why nawe hasira ,zilikupanda ukajibu mapigo bila kujitambua na ndio maana mpaka leo unajutia.
Tafuta kiongozi wa dini ya wazee wako hasa yule wanae mheshimu na kumkubali mwambie kila kitu then muombe uongozane naye mpaka kwenu akuombee msamaha na wewe ujinyenyekeze to the maximum. Baada ya hapo wakikusamehe toa neno la shukrani na wakigoma kutoa msamaha mbele ya kiongozi wao wa dini ondoka zako kwa amani kapambanie maisha yako ya baadae.
Na kwa huyo bi dada au malaika mlinzi kama ulivyosema kweli mchukulie kama malaika aliyetumwa na BWANA kwa ajili ya kukuokoa katika hatari uliyokuwa nayo hivyo mpe heshima yake yeye na huyo boyfreind wake katu usije kuwa chanzo cha uvujifu wa.mahusiano yao unless otherwise itokea wao wenyewe bila wewe kuwa chanzo.
Pole tena na MUNGU yupo atakusaidia.
 
Hongera sana kwq uthubutu mkuu, mzazi hata kama mzazi akileta ujuaji na kutingwa huku tunamsukutua tu. Hapo haina haja ya suluhu wala nn maisha yanakwenda na kila kitu kina mipaka, ndo mana kuna mzazi na MUNGU

Kuhus DEmu usimtongoze mkuu ila akikupa chukua ila usijitoe ufaham kumuomba utajiharibia. Huwez jua yote anayofanya kama kajipa udada au umama. Usije kutongoza ukajiharibia hata option iliyopo wakati huo unaanguka tena. Maisha ni up(s) and down (s).

cc. Kapeace
Q
 
Kwa mzazi asirudi mkuu, yeye akomae mzazi ajiheshimu na ajue mipaka kti yake na Mungu. Mzazi akijiona mungu na mungu yupo anakula kibano tu
 
Huko juu inasemekana kajamaa huenda kanatunga hizi story zake,

Ana wazazi mcharuko hasa mama ni kichomi
Baba mtu ni mwanaume aliezidiwa nguvu ya maamuzi na mkewe maana kwa hadithi yake mshua alikuwa anapata kichapo enzi hizo

Akawaombe msamaha hata km atakusanya ukoo mzima, akishapata radhi aondoke akaendelee na mapambano ya kimaisha

Huyo dada hatakiwi hata kumuonyesha matamanio ya kingono amkumbuke mchumba wake na jinsi alivyotambulishwa kuwa ni ndg wa bamdogo, atafute mpenzi na aache kujilegeza kwa wanawake wa watu..... atakufa
 
Mimi nilichoambulia tu ni pale uliporuka teke la hewani kama van dame kutua tu ukakuta kifua cha mzee kinazembea zembea ukakiunganisha babu wa watu kule any way ndugu yaliyokutokea wewe yamewatokea wengi sana, kuna wakati wazazi wanakosea sana sana
Lakini kwa tamaduni nyingi bado zinasema mzazi hakosei na wewe ishi humo
Pima upepo ni nani anaheshimiana sana na wazee wako kisha ongea nae na ujirudi hata ungekua wewe kwa hilo teke la van damme lazima ungenuna

Kingine acha kabisa kabisa kujaribu kutembea na huyo dada ,hisia zinadanganya sana na wanawake viumbe wa ajabu unaweza kudhani kakuonyesha dalili za kukutaka ukiingia tu kichwa kichwa heeeeeeeeeh

Ugonjwa wa moyo utarudi huo
 
Mzazi sio muhimu sana.. kuna wahuni wamezeeka na kuwa wazazi. Hao sio wa kuhesabia sana mkuu.. muhim ni kuamini kwamba makosa kila mtu anafanya. Suala la kufanya makosa makusudi kisa mzazi hakosei halipo. Mzazi akikunyea usoni hata kama mzazi sio kosa?

Kuna jamaa mmoja hapa mtaani baba yake ni fundi. Amekuwa na tendency na kupokea tenda na kula hela nusu alafu kazi ikibakia kuwa kimeo analazimisha mwanae akaifanye hata kama haina hela. Amekuwa anamuachia radhi kila wiki walau mara 1 kwamba asipoganya kazi zake hana radhi nae. Na jamaa bado anadunda mpaka leo hii
 
Kwenye hadithi muhusika ni km anateswa nq hiyo hali ya kutokuwepo maelewano na wazazi wake, ila angekuwa na maamuzi magumu km kina sie aaah unanyamaza km washakuzika
 
Ingawa ni ngumu kuhusu wazazi wako jitahidi tu kuachana na kuwatafuta au kuwasiliana nao utajitesa bure.....

Umeshatubu na una nia ya dhati, cha kufanya endelea kuwaweka kwenye maombi na lile fungu ambao ungelitenga kwaajili yao kama mngekua na mahusiano mazuri to sadaka tu, tafuta wahitaji na toa msaada....

Kwa mfano
1. unaweza mashati ya shule ukawapa watoto wenye mazingira magumu
2. Ukanunua sukari kilo 50 ukazifunga hata kg 2 ukaenda kugawa mfano ward ya wazazi waliotoka kujifungua sababu wanakunywa sana uji etc....

Every time ukitoa sadaka hiyo ombea amani yako binafsi na familia yako ijayo na maisha yenye afya kwa wazazi wako.....
Huhitaji kuwa karibu na wazazi wako, they have been toxic toka ukuaji wako, hawawezi kubadilika sanasana watakuharibia familia yako ijayo
 
Unaanza kuhanagaika kurudi kwa wazazi wako ili iweje.kwanza ilibidi wao ndio wakuombe msamaha kwa waliyokifanyia mpaka unakua Wangekuwa na busara wangeelewa shida ulizopitia. The fact kwamba wamekunyanyasa toka mdogo ni ishara kuwa hawakupendi hivyo achana nao. Wapotezee wao wenyewe watakutafuta wakishajua unamaisha mazuri mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…