Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Mdogo wangu.

Biblia inatoka Wajibu Kwa wazazi na watoto.
Kwa watoto Mungu anatoa AMRI kuwaheshim wazazi .

Kwa wazazi Mungu anahitaji awapende watoto.


Kama Ulivyopiga Maombi ya Mungu Shuka, usiposhuka, nakufata hukohuko juu.


Vita ya wazazi wako sio ya Mwili, MUACHIE MUNGU NA UENDELEE KUMUOMBA MUNGU HUKU UKITOA SADAKA NA ZAKA, NA KUSAIDIA WATOTO YATIMA, NA MASIKIN NA WAGONJWA .



Jambo nililonalo uhakika, IPO SIKU WAZAZI WAKO WENYEWE KWA AKILI YAO TIMAMU, WATAKUTAFUTA.


Kuhusu Huyo DEMU, endelea kumuweka kwenye Friend zone , usimtongoze , Acha Nature yenyewe ifanye kazi, maana inawezekana yule Mchumba wake ni bwana tuu naye ana mwanamke , au akawa kweli ni mchumba wake, ila Nature imeshakataa wao kua wanafamilia
 
Kwa tafsiri nyingine inawezekana huyo mama yako ni mshirikina au mchawi kbs na alisha muathiri mzee wako pia, na inawezekana ulitakiwa utolewe Kafara alipo shindwa ndio chuki ikajengeka, lkn Mungu alikua pamoja naww na ndio maana ulipo mkumbuka katika maombi akakuletea Malaika mwokozi....km vp ww achanao tu maisha yaendelee, ipo siku watakuja kutubi kwa walio kutendea
 
pole sana kwa madhila uliyopitia,mshukuru MUNGU kwa yote.kamwe USITHUBUTU kumtongoza hata kwa UTANI huyo mwanamke aliyekusadia. kuna tofauti ya upendo na mapenzi, tambua kuwa UPENDO wake kwako ni wa kirafiki zaidi siyo kimapenzi. na hata ikitokea hisia za mapenzi acha aanze yeye kukuonyesha, otherwise big NO!
 
Dah mkuu pole kwa uliyopitia na hongera pia kwa kutoboa gizani

Sema hapo kwenye mdada mrembo umenitisha maana kuna mdada wa kishua hapa nakula kwa macho nisijemwaga sera kumbe ni malaika mtuliza ghasia huko mbeleni.
 
Mkuu, Hakuna Mwanadamu mkamilifu. Nimetambua anguko langu la miaka mitatu iliyopita na nimeshaweka juhudi za kutosha kutafuta utatuzi na hivi bado naendelea Kupambania
 
Haya mambo yapo sana kwenye familia. Zaidi ya msamaha wa mdomo, endelea kujishughulisha na kujihusisha na mambo ya hapo nyumbani kwa kupitia wanafamilia wengine mfano wadogozako au wakubwazako kama wapo au ndugu yeyote aliyeko pale nyumbani. Kama anasoma msaidie mahitaji muhimu, kama yupoyupo mfanyie kitu cha kujishikiza kimaisha nk. Kupitia hao utapata mlango tuu wa kuingia kwa wazazi.
Huyu dada malaika asikufanye mtumwa wa kimawazo na kihisia kisa alikusaidia. Kaa nae kitako cha mazungumzo serious Mwambie ukweli wako kwenye mapenzi. Kama kweli unampenda mwambie uko tayari kumwoa ila kama unamtamani au bado unazingua mjini mwambie kipande cha mapenzi kisionekane maana ni dadayako na wifi yake amfahamu kama yupo. Weka malengo mazuri ushakua, ukivuruga hapa kutazuka uadui mkubwa na utajisikia hatia mbaya.
 
Asante sana Mkuu kwa Ushauri .
 
Achana na mawazo ya ngono kwa huyo binti, wanawake wanatumia hisia sana , wewe tumia akili kumkwepa kuepusha matatizo maana bado unajitafuta.

Kama umetumia mbinu zote kwa wazazi na imeshindikana, jipe muda na uwape na wao muda ila usiache kuwaombea kwa imani yako.

Wazazi hawajuagi tu ila kufoka foka na kupiga hovyo watoto hata kwa kosa dogo sio malezi bora, kunamfanya mtoto asijiamini ama lah akikua atataka apate uhuru mapema sana na kuharibikiwa.
 
Eti umpige kofi mama na umpige teke baba?.

Binafsi nasema hata kama umefanikiwa saana lakini Wazazi uliwakosea saana.

Nenda kawaombe radhi mwenyewe siyo kutumia watu.
 
Huo ushauri wa kukaa kitako kumchana binti makavu ilhali binti hajawa wazi kua anamtaka ni kiburi cha mafanikio hicho.

Aishi nae kama rafiki na kama ndgu, hizo anazosema green light si ajabu kwa binti ni mambo ya kawaida kumfanyia rafiki ila yeye kwa sababu anampenda binti basi anaona kama binti kazama mazima kwake.
 
Eti umpige kofi mama na umpige teke baba?.

Binafsi nasema hata kama umefanikiwa saana lakini Wazazi uliwakosea saana.

Nenda kawaombe radhi mwenyewe siyo kutumia watu.
Hujawahi kukutana na wazazi watukitu wewe.

Yaani jamaa angeruhusu apigwe gongo la kichwa kisa alieshika gongo ni baba??
 
Pamoja na kwsmba watoto wsnapaswa kuwatii wazazi wao, lakini wazazi wamekatazwa wasiwachokoze watoto wao.

Kikubwa acha kuwaza kama una baba au mama maana imeandikwa LAANA ISIYO NA SABABU HAIFANIKIWI. Yaani wakuchokoze, wakutese, wakunyanyase kisha wakulaani hakuna hiyo kitu.

Ishi kivyako na usiwasiliane nao tena. Mungu amekutenganisha na wouldbe kifo chako kwani lile gongo lingetua kichwani, leo usingeandika haya.

Pambana utoke kimaisha. Mapenzi yatakuja yenyewe
 
Kwenye mila zetu anayemtaka mwenzie waziwazi ni mwanaume na si mwanamke. Huyu bwana asipoangalia anageuka mfungwa wa kihisia kwa huyu dada. Uliona wapi kwa mwanaume aliyekamilika anapigwa mabusu na mtoto wa kike halafu hakuna kitu kinatokea? Kwa namna hii Hata kuendesha uhuru wake kimapenzi itakuwa anaogopa au anafanya kwa Kiti Cho kwa kumhofia akijua itakuwaje. Muhimu mstari ujulikane uko wapi kwa usalama wa wote wawili hapo baadae.
 
Kwa maelezo yako, ingawa ninekosuma mpaka ulipompiga mamako na babako nikaachia hapo, unaonesha ulilawitiwa huko boarding na chuo kikuu.

Wacha ushoga, fanya toba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…