Tumbiliwaulaya
JF-Expert Member
- Nov 22, 2020
- 280
- 435
Zipo sababu kadhaa zinazowafanya makada wa CCM kuendelea kuing'ang'ania katiba iliyopo isibadirishwe na iendelee kuwepo kwa jinsi ilivyo. Kubwa kuliko zote ni maslahi ya chama chao, kila mwana CCM anaangalia na kupigania kwanza maslahi na uhai wa chama cha mapinduzi kabla kitu kingine chochote kile nijuavyo mimi maslahi ya nchi yapo nyuma ya maslahi ya CCM.
Katiba tuliyo nayo kimsingi imeweka madaraka makubwa sana kwa Rais wa nchi ili aweze kukilinda chama kwa njia yoyote ile bila kuathiriwa na katiba na sheria za nchi,na ili CCM iendelee kuwa chama dora ni lazima Rais wa nchi awe Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,pili kushikamanisha kwa njia moja ama nyingine nyadhifa za kiserikali na chama cha mapinduzi kwa njia zisizokuwa halari ki katiba mfano wakuu wa wilaya na mikoa.
Kukataa kwa makusudi kutii hukumu kadhaa za mahakama mbalimbali kuhusu uhuru wa watu kugombea nafasi za kisiasa wakiwa kama wagombea binafsi,hili lina athari ya moja kwa moja kwa CCM kwani inajua wazi kuwa udhibiti wa nidhamu kwa wanachama wao utakuwa mgumu hivyo kupelekea wanachama wao kuwa huru kifikra katika kufikia maamuzi mbalimbali, jambo hili amelikiri mzee Ally Hussein Mwinyi katika kKtabu chake hivi karibuni kuwa Mwalimu alitaka nchi kuwa na wagombea binafsi kamati kuu ilikataa ikihofia uhai wa chama hivyo huu ni ushahidi tosha kuwa hapa maslahi ya chama yalitangulizwa mbele dhidi ya haki za raia na nchi yao.
kutokana na hayo mwalimu aliwahi kusema katiba ya nchi yetu inaweza kumfanya Rais wa nchi hii kuwa dikteta kwa kuwa imempa madaraka makubwa kupita kiasi,kwa hali hiyo tunaishai kwa kudura za Mwenyezi Mungu.
katika hali kama hiyo ni nini basi kinawafanya hawa wana CCM kung'ang'ania katiba hii wakati wanajua tunaishi kwa utashi wa mtu mmoja na si wa kitaasisi kama ilivyo mataifa mengine?
hebu tuone mifano michache ya mambo ambayo yame waumiza wanachama nguli wa CCM kutokana na muundo mbaya wa Katiba yetu. Kuvunjwa kwa haki ya faragha katika miaka mitano iliyo pita kume waathili sio tu watu wa kawaida bali hata Mawaziri, Wabunge,na wana chama nguli kama Mzee Makamba, Nape Nauye na wengine wengi, tumeshuhudia wakina Nape na Makamba waki tambaa kama watoto wadogo kuomba msamaha kwa mtu ambae dhahili alikuwa amefanya kosa la udukuzi na kuingilia haki za faragha za raia wake.
Uvunjwaji wa Katiba wa makusudi uliokuwa ukifanyika bila kukemewa na mtu yeyote kwa hofu ya kumuogopa mtu mmoja mwenye madarakayaliyo kithiri. Kufungwa midomo watu wote hakuna mwanaume aliye kuwa anasema ng'we wote tulirudishia mikia ndani kama vijibwa vilivyo poteza dira.
yapo mengi ndugu zangu wengine watawakumbusha bado mna hamu?
The bulldoser hamtamsahau.