Ni nani alikuwa bora zaidi, Drogba Au Eto'o?

Unamfahamu etoo wakati anacheza Real Malorca kwa mkopo? Waulize Real Mardlid.

Etoo wakati anaenda barca, barca ilikuwa iko hovyo(ilikuwa inazidiwa hadi na valencia ya benitez) na wakati huo pia chelsea pia ndio inaibukia kwenye ushindani badala ya roman kuinunua.

Viwango vya barca vs chelsea havikuwa na tofauti kiivyo.

Lakini mpaka muda huo barca ilibebwa na wachezaji watatu, gaucho, deco na etoo kabla ya gardiola.

Hivyo kwa hii hoja yako Etoo ni bora mara mia kuliko drogba.

Uzuri wote walihamia hizo timu kwa nyakati moja(hawakupishana sana)
 

Kwahiyo Chelsea aliyocheza Drogba ya kina Makelele, John Terry, Ashley & John Cole, Cavalho, Lampard, Joy Cole then Malouda ilikuwa average isiyo na uwekezaji mbele ya Intermilan ya kina Cambiasso na Balotelli aliyocheza Eto'o ?
 
Tunapozungumzia magwiji wa soka Africa huwa tunasimama dakika moja huku tukipiga saluti kwa Jay Jay Okocha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Etoo alikua Bora zaidi ya Drogba ila baadae Drogba alipambana akawa Bora Kama etoo na zaidi labda kwakua wakati Drogba anazidi kuzeeka alikua anazidi kuwa hatari huku etoo alikua anapungua ukali....ila Etoo ni Bora zaidi ya Drogba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…