Ni nani hasa wa kubadili dini?!

Ni nani hasa wa kubadili dini?!

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,750
Reaction score
2,283
Linapokuja swala la kubadili dini katika mahusiano, Wanaume wengi wa kiafrika huwa inakuwa ngumu sana. Na pale inapotokea kwa mwanaume huwa wengi wetu tunamshangaa kidogo mwanaume anaebadili dini yake kumfata mpenziwe wa kike.! Ila kwa mwanamke kumfata mwanaume ni kama kawaida na wengi wanaona inatakiwa kuwa hivyo.

Kwa upande wako vipi ikitokea?, uko tayali kuhama kwenye imani yako ulipo zaliwa ukiabudu kwa ajiri ya Mapenzi?!.
 
Wajuzi wa mambo japo siyo rasmi ila watu hunong'0na kuwa kiukweli, Mwanamke HANA DINI, bali humfuata mume. Argument hii sina hakika kama ni valid hadi leo au ni enzi hizo za upagani
 
Wajuzi wa mambo japo siyo rasmi ila watu hunong'0na kuwa kiukweli, Mwanamke HANA DINI, bali humfuata mume. Argument hii sina hakika kama ni valid hadi leo au ni enzi hizo za upagani
Nadhani hii statement bado ipo wazi na huo ndo ukweli!
 
binafsi kabla ya kuanzisha mahusiano mapya dini huchukua nafasi sehemu yake tena kubwa tu
 
Mo sibadili ng'o... na either mawili... abadilishe yeye... au mahusiano kuvunjika
 
Binafsi siwezi kubadili dini kisa Mapenzi. YESU ni bora kuliko hiyo ndoa
Kwani bi Dada wewe kwako Yesu ni Mungu au mtoto ??
arton617.jpg
 
Kaanzishe uzi wako tujadili huwezi kula kona.
Changia kuhusu mada
Una hasira hivi hata huyo "Yesu" unamtumikiaje, tunaoamini kuwa Yesu ni mwokozi wetu hatupo hivo tuna roho ya usikivu na uvumilivu,na hivo ndio hunioni unanijibu hivo je ungekuwa unaniona si ndio ungenitukana kama sio kunipiga kabisa.
 
Kila kitu maamuzi na kuamua pamoja na mpz wako. Kwani kuna ubaya gani mwanaume kumfata mwanamke? Hv siku hizi bado mnaoaga dini au mnaoana kwa vile mmependana? Kama kila mtu hataki kumfata mwenzie mbona kuna ndoa za serikalini au bomani halafu kila mtu anaendelea na dini yake. Kasheshe kwa watoto mtaamua wafate dini ya mama au baba ila wakikua watajua pa kufata. Cwez nikamuacha mpz wangu niliyetoka naye mbali kwenye shida na raha tupo wote sababu ya dini tu? Tunafunga hata bomani shida ni mapenzi ya kweli na ya dhati
 
Hii mada inanigusa moja kwa moja.although naamini kwamba upendo Ni kila kitu kwangu.upendo Ni zaidi ya dini zetu.makabila.hadhi za kiuchumi Na n.k.so far siku ya kiama kila mtu atasimama kivyake kujibu mashtaka wala huwez simama Na mkeo au mmeo.km mnapendana kila mtu asali kivyake Na Maisha yaendelee.binafsi kwenye suala la watoto kwangu naamini dini ni imani ambayo Ni lazima uikiri mwenyewe hivyo cwez kumlazimisha mwanangu afuate dini yangu Bali akiwa mkubwa atachagua pa kwenda.zamani dini ilikuwa sheria lkn baada ya yesu kristo unaamua mwenyewe kwa Moyo Na kinywa kwamba yesu Ni ndimi njia ya uzima..MWISHO NITAOA MWANAMKE NIMPENDAE NA SI DINI YAKE
 
Una hasira hivi hata huyo "Yesu" unamtumikiaje, tunaoamini kuwa Yesu ni mwokozi wetu hatupo hivo tuna roho ya usikivu na uvumilivu,na hivo ndio hunioni unanijibu hivo je ungekuwa unaniona si ndio ungenitukana kama sio kunipiga kabisa.
Hivi wewe una nini lakini?
Mimi mabishano ya dini sitaki
 
Kwanza unatakiwa kutambua hakuna uhusiano wowote kati ya ndoa kudumu na dini.

Unaweza kuoa mtu wa dini Yako na ndoa isiwe na furaha

Pia unaweza kuoa mtu asio wa dini Yako na ndoa ikadimu

What I want to say usikubali kumpoteza mtu muhimu katika maisha Yako kwasababu ya dini.

Angalia uzito nani ana access ya kubadiilisha dini kwa harakati bila misunderstanding kubwa kati ya me au ke

Ila hapa jitahidi sana kuangalia mwanamke Ambae utabadilisha dini ili umuoe

Amekupenda kweli??
Atakuvumilia??
Mnaendana ??
Kama jibu ni ndio badilisha dini haraka

Mimi nilikuwa muislamu pure kabisa ila nilikutana na huyu mke wangu huu mwaka wa 15 nilibadilisha dini na kuwa mkristo tena msabato

Mambo yalionifanya nibadilishe dini
Kwanza nilimkuta akiwa bikra chuo mwaka wa tatu

Amewai kunisaidia sana financially Yani nilikuwa sina msaada yeye ndio alikuwa assistant kwangu

Alinikuta nalala chini sina hata godoro ila mpaka Leo Nina nyumba tatu
Yani bikra yenyewe nilimtolea chini kwenye sakafu

Ni mwanamke mwenye akili nyingi anajua budget mvumilivu Yani mpaka raha

Kwaiyo hakuna mtu specific kubadiilisha dini inategemea tu na nyie mtaamu vipi...

Dini ni njia ty
Uislamu uarabu
Ukristo uzungu
 
Linapokuja swala la kubadili dini katika mahusiano, Wanaume wengi wa kiafrika huwa inakuwa ngumu sana. Na pale inapotokea kwa mwanaume huwa wengi wetu tunamshangaa kidogo mwanaume anaebadili dini yake kumfata mpenziwe wa kike.! Ila kwa mwanamke kumfata mwanaume ni kama kawaida na wengi wanaona inatakiwa kuwa hivyo.

Kwa upande wako vipi ikitokea?, uko tayali kuhama kwenye imani yako ulipo zaliwa ukiabudu kwa ajiri ya Mapenzi?!.
Kwanini mbadili dini, si kila mtu abaki na dini yake?
 
Back
Top Bottom