Ni nani huyu Cool 9 Jamani?


hapa kuna jamaa anapiga mtaa mzima, nani anajua background ya huyu bwana? anajulikana Tz nzima.
 
Kule kwetu kulikuwa na Pawa Mwanza, pawa Mabula, Pawa Sozia na Pawa Malimao

Walikuwa wanapiga hadi chai maharage zinaanguka

loh.....almanusra nidhani nilikuwa msumbiji...
Labda alikuwa mbabe wa mtaa wao.....

Anyway mleta uzi, tiririka basi na viroja vya huyo jamaa
 
Huyu jamaa alikuwa mbabe kweli mara ya mwisho nilikutana nae osterbay polisi miguu ilikuwa imemvimba na baada ya hapo nikaja kusikia amefariki,wadogo zake wote walikufa kwa bunduki
 

point of correction sir,isomeke alipigwa risasi
 
Huyu jamaa alikuwa mbabe kweli mara ya mwisho nilikutana nae osterbay polisi miguu ilikuwa imemvimba na baada ya hapo nikaja kusikia amefariki,wadogo zake wote walikufa kwa bunduki

tupe stori zake kaka ilikuwa mwaka gani hiyo na alikufa kwa ishu gani mani testa tupe unavyovijua bhanaaa!! wadogo zake we kumbe unawjua ni kina nani hao?
 

Mjomba tujuze zaidi mbona unatuachia njia panda tupe historia yake basi!!!!
 
Grand Master Dulla hivi unakumbuka siku peppe kalle alipokuja dar mara ya kwanza pale friends corner? nakumbuka ilikuwa enzi zile za kibao cha hidaya basi huyu bwana ndo mara ya mwisho kumuona machoni. alitumika kama baunsa manake alikuwa anapiga vipisi usimpimie.
 
Last edited by a moderator:
Alikuwa maarufu sana Iringa ingawa hapa Dar alikuwa anakaa Kimara maeneo ya Kibo wakati ule ukienda disko na demu mgeni lazima wakupore kuna jamaa yangu alitoka dar na demu wake akawa anataka kumpora bahati akakutana na rafiki yake ambaye alikuwwa maarufu iringa ndio akamsaidia akamuita akamtambulisha huyu jamaa yangu toka dar anakaa kimara aliposikia hivyo akamwambia na yeye pia kwao ni kimara maeneo ya kibo.
Mkono wake mmoja ulikuwa kama umelemaa wanasema alipigwa shaba na dereva wa magari makubwa .kaka yake sikuwahi kumshuhudia ila nasikia alikufa kwenye tukio la ujambazi.
Iringa kulikuwa na wababe wengi kama kina domi na wengineo ila wengi wametangulia mbele ya haki
 

nakumbuka hiko kibao kibao kilitoka mwaka 92 pamoja na wimbo wa roger milla hivyo kama kuja bongo itakuwa alikuja 92 mwishoni au 93 hivi tupe zaidi gfsonwin
 


I see huyu chalii alikuwa ni noma, yeye pamoja na ndugu zake kina Shedadi, Ayat na dada yao alikuwa anaitwa Chola. Kwao mtu aliyekuwa ametulia alikuwa mdogo wao alikuwa anaitwa Ally Tungu. Utemi wa kuchukua mademu kinguvu alikuwa haufanyii disco tu bali hata mitaani, akimtaka demu halafu akatae maisha yake yatakuwa magumu sana hivyo wengi walikuwa wanakubali yaishe.

Alipigwa risasi na dereva wa lori baada ya kusimama mbele ya lori hilo na kulizuia lisiondoke mpaka atake yeye, akamkuta mzee wa kihehe amedata zaidi yake akamuwasha. Kaka yake Ayat alifariki kwenye tukio la ujambazi.

Nakumbuka siku moja disco alikuja akakuta watoto kibao ambao walikuwa na kiingilio pungufu wako nje akawaambia leteni hela mlizonazo nitawaongezea muingie wote. Basi watoto wakampa hela zote baada ya hapo jamaa akazama ndani (na alikuwa halipi kiingilio, muulizeni Papaa Felicia Chaula wa FM academia anamfahamu vizuri).

Wale watoto wakawafuata Polisi wa patrol wakamshitaki. Polisi kuja jamaa akatoka akawaambia kwa ukali kuwa wasimsumbue yuko kwenye starehe zake kama wana shida naye wamfuate kesho, Polisi wakaondoka wamenywea. Dah!
 
haya na nyie wa dodoma njooni na stori za black madonna, sasa
 
na mimi nauliza yule mtemi wa mitaa ya sinza miaka ile ya 2000-2006 alikuwa anaitwa "DAME" kashatoka jela?kuna jamaa aliniambia yupo gereza la segerea akinyea debe.
 
Nilichokuwa namfurahia Cool-9 wakati huo nikiwa Primay, watoto tukienda SAMORA kuangalia LIPULI, basi mnasikilizia Bratha KUL aje akifika wote mwaingia BURE ATI!!!

 
tupe stori zake kaka ilikuwa mwaka gani hiyo na alikufa kwa ishu gani mani testa tupe unavyovijua bhanaaa!! wadogo zake we kumbe unawjua ni kina nani hao?

nilikutana nae mara ya mwisho mwaka 2002 ila aliniambia kuwa alifariki sikumbuki aliniambia ni mwaka gani,jamaa walikuwa wanaishi maeneo ya kitanzini mkoani Iringa akiwa yeye kaka yake shedadi wadogo zake hayati,ambae aliuwawa kwenye tukio la ujambazi kwenye magodown ya RTC mlandege,jamaa mkono mmoja ulikuwa na jeraha la risasi baada ya kutwangwa na dereva wa malori,aliwasumbua sana polisi pale Iringa
 
Mkuu wewe kweli unamnyaka vizuri jamaa alikuwa kama mburushi
 
 
Version hii naona ndio imekua kamili zaidi. Enzi zileee! Yule kulunaini mie nilidhani alikua maarufu iringa tu kumbe mpaka daslama...ndio maana alikua anaonea sana iringa alikua anaona wote washamba tuu.
Namkumbuka pale samora always alikua anaingia bure na walikua na katimu chao hivi ka vijana wa kitanzini nimekasahau jina.
Pale disco toto ya ile klabu ndani ya samora enzi zile inatamba "yekeyeke timoroo yekeyekeeeee...vikuku vinanukia aaaaaah...." mkiwa na bahati anafanya ubabe wake mnaingia bure, basi fulu heshimaa.
Tukio alilokufa kaka yake Ayati na vijana wengine kwa kupigwa risasi lilikua '91 au '92 pale RTC mlandege,stori zilienea kua mlinzi yule alikua na risai moja tu ikabidi afanye timingi apige shot moja tuu ikawaunganisha wote watatu hahaha...ilidaiwa kuwa Cool 9 nae alikuepo ila alifanikiwa kutoroka.

Siku hizi bana MABAUNSA ni wenye pesa tuu,wenye misuli kazi yao ulinzi tu...CHANGE!
 

Huyo Jamaa namnyaka sana, alikuwa shombe shombe hivi.... Alikuwa ni mbabe sana miaka ya 80 hata mapolisi Iringa walikuwa wanamgwaya..... Mpaka leo sielewi mapolisi wa wakati ule walikuwa wanamwogopa kwanini.... Iringa tulikuwa hatuna amani huyu jamaa akiwepo... Kama ni disco pale Ruaha international ama Soweto kama mnaenda na mademu hakikisheni mnaenda group la watu walioshiba sio kwa kula tu bali kimazoezi.... Na mkubaliane kabisa kama lolote litatokea hakuna kukimbia.... Nimeshuhudia mara kibao watu wanakimbia na mademu wao.... Maana tatizo la Cool 9 lilikuwa anapoanzisha vagi huwa haliishi mpaka ashinde ugomvi.... Mikutana linaanza upyaaa.. Ukweli alikuwa ni mtu wa mazoezi na alikuwa anatisha sana na makarate, makung fuu na ngumi za ulingoni alikuwa anaziweza.... Sina kumbukumbu kuwa alishawahi pigwa kisawasawa akome tabia ya kupora mademu kwa nguvu ...Nashangaa kipindi hicho hakukuwa na kesi za ubakaji nadhani angekuwa nazo nyingi saana. Nakumbuka Yeye, mdogo wake Shehedad na Dada yao wote walikuwa ni balaa sana .... Akiwa Dar watu walikuwa wanapumua kidogo na kunakuwa na kaustaarabu kwenye kumbi za starehe.... Alikuwaga na Girlriend wake alikuwa anaitwa Peresi naye alimfundisha kuzipiga kama yeye..... Ila alishatangulia kwenye haki...Alikufa akiwa tayari kilema wa mkono kutoka na kujiingiza kwenye mambo ya wizi kwa kutumia ubabe wake.... Cool 9 alikuwa Nouma sana huyo jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…