Jamani naomba kuwauliza swali linalonitatiza sana.
Miaka ile ya themanini wakati mi niko mdogo kule Kinondoni kulikuwa na tajiri mmoja mwenye magari mengi aina ya scania 111, jamaa mwenyewe alikuwa anaitwa MWANAMBOKA na mascania yake tulikuwa tunayaita mascania ya Mwanamboka.
Huyu jamaa ni maarufu sana Kinondoni pale, sasa miaka ya 2000's akaja akajitokeza binti mmoja anayeitwa KHADIJA MWANAMBOKA, sasa nauliza huyu Khadija Mwanamboka ni mwanawe au ni ndugu au ni jina tu limefanana? Maana huyu Khadija anaonekana ni mwarabu na yule mzee mwenyewe kama jina lake linavyoonyesha ni mswahili ila sijui ni wa mkoa gani wala kabila gani.
Hivyo jamani kwa yeyote yule mwenye kumjua huyu mzee atupe historia yake na ya familia yake mana alikuwa maarufu sana enzi hizo dsm.