Ni nani Mmiliki Wa Blog Hii Millardayo.com?

Kifurukutu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
4,641
Reaction score
6,694
Habari Jf

Nimekua nikifuatilia kwa ukaribu sana habari kutoka blog mbalimbali Tanzania, mwisho wa siku nikalizishwa na kuiamini MILLARDAYO.COM kama blog inayocover habari za aina zote ndani na nje ya nchi.

Kilichonifanya kujiuliza, hii blog pendwa ni nani mmiliki wake?

nimejiuliza sana kutokana na ukimya wa blog hii huru kutokuripoti habari za tunza za EATV zilizofanyika usiku wa tarehe 10.

Vipi wakuu, mwenye uelewa wa hii blog inamilikiwa na nani ajaribu kunielekeza.
Pia inasimamia vitu gani hadi iweze kuripoti habari yako kwani kwa tukio la jana ndio lilikua tukio kubwa katika burudani hapa nchini lakini likasusiwa na millardayo kitu ambacho si kawaida yake!

Mwisho, pongezi nyingi ziwafikie East Africa Tv kwa kufanikisha EATV AWARDS 2016
 
Inamilikiwa na millard ayo mtangazaji wa clouds fm,ila hii blog sio huru kama alivo mmiliki wake japo naona ni kukosa weledi tu,sawa EATV ni washindani wa clouds lakini sikutegemea kama huyo jamaa angekuwa mnazi kiasi hicho,hata habari za jide huwa haandiki,hizo ndo akili za waandishi wetu wa habari kanjanja.
 
Nikweli jamaa anaangalia unga wake
 
inamilikiwa na Millard ago mfanyakazi wa cloudz FM. kwa sababu wana beef haruhusiwi kuripoti
 
HATARI SANA

Huu ukiritimba utaisha pale tutakapokuwa na uwekezaji zaidi kwenye tasnia ya habari na siyo kuitegemea Media moja tu hadi wakuu wa nchi POMB@ na SHISHA wameifanya ndiyo media ya TAIFA na kuitelekeza TBC sijui lini na ninani wa kubadilisha mifumo hii kandamizi

Leo hii msanii akitofautiana kidogo tu na media hii tunamsahau kwenye sanaa hakika ukombozi unaitajika. kuna watu wamekuwa miungu watu hapa duniani..

Wa kulaumu siyo (Mtu wangu) wa nguvu MILLARD AYO maana na yeye anaogopa kumwaga UNGA na anakumbuka katokea maisha ya shida kule ..(A-town) nadhani ata yeye inamuuma ila afanyeje..???

Imeletwa kwa hisani ya kijukuu cha hitler Adolph hitler jr
 
Au ndo yale kuwa mtoa ofa ndo mchagua wimbo.............mtoa ofa akicheza mpewa ofa lazima nae acheza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…