kikokotoo kipya
JF-Expert Member
- Dec 18, 2018
- 441
- 488
Nimekuwa nikishangaa sana, serikali imejenga Uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa,kwa mabilioni ya fedha.Lakini imeshindwa kununua kibao cha kisasa kinachoonesha namba ya mchezaji anayepaswa kutoka na anayepaswa kuingia kwenye pitch,wakati wakubadilisha wachezaji, pia muda wa nyongeza.Wamebaki na vibao vya zamani vya kubandua na kubandika namba.
Mara kadhaa utasikia takwimu nzuri za mapato ya mechi moja tu ya Simba na Yanga.Mamilioni ya shilingi huingizwa kwa mechi moja tu,ingawa timu husika huambulia kiduchu nyingi ya kiasi kilichopatikana huishia kwenye makato ya TFF na tozo ya uwanja.Je TFF hawezi kutenga kiasi cha mapato wanayokusanya katika mechi hizo kununua Kibao cha kisasa na kurekebisha sehemu wanapokaa wachezaji wa akiba na benchi la ufundi?,iwe ni TFF au serikali ama wote kwa pamoja hawezi kweli kurekebisha mambo madogo kama hayo ili angalau yafanane na Uwanja wa taifa?
TFF,hupokea RUZUKU kutoka FIFA na serikali nayo ina bajeti ya wizara ya michezo,pamoja na Tozo za mechi wanapotumia uwanja wa taifa,Je hicho kibao na sehemu wanapokaa benchi la ufundi vina gharama kubwa sana kiasi cha kuwashina kununua?, au ndio kutojipenda na kutojijali kwa Waafrika au watanzania.Labda tunsubiri mh. Rais agundue na atoe agizo au atoe msaada?
Siamini kama TFF hawana aibu kiasi cha mashindano ya Vijana kuanza tukiwa na udhaifu wa vitu vidogodogo,ambavyo vinatufanya tuonekana watu wa ajabu ajabu hivi.