Elections 2010 Ni ndani ya Tanzania pekee....

Elections 2010 Ni ndani ya Tanzania pekee....

Mujuni2

Senior Member
Joined
Jun 11, 2008
Posts
142
Reaction score
3
Ni ndani ya Tanzania pekee, yaweza tokea yafuatayo:
1. Kiongozi wa kisaiasa anaweza kukejeli wapiga kura na bado akashangiliwa.
2. Wanasiasa hawawajibiki kwa waliowachagua.
3. Uraia unakuwa muhimu pale tu, mhusika anapogombea nafasi ya kisiasa.
4. Chama tawala hutumia kodi za wananchi kwa maslahi ya kisiasa na hasa uchaguzi.
5. Chama cha wafanyakazi(walipa kodi) kinasalimu amri kutoka serikali kuu.
6. Wabunge wasiowajibika kwa wapiga kura huchaguliwa kwa miongo mfululizo.
7. Afya ya Rais inalinganishwa na nyaraka za siri za serikali.
8. Mfumuko wa bei za bidhaa (mkate)hauambatani na maandamano ya kupinga.
9. Vyama vya upinzani hupingana badala ya kuungana.
10. Chama anachotoka mgombea kinapewa nafasi kubwa, kuliko uwezo binafsi wa mgombea.

..Waweza ongeza zako kwenye list hii.......
 
Haya mambo yapo kwingi zaidi ya tanzania tu. Kenya, uganda, zimbabwe, libya, urusi, n.k. Haya mambo yapo. Tofauti na wenzetu hao sie upumbavu wetu tunautekeleza katika misingi ya amani zaidi
 
kingi
lakini hili la kukataa kura za watu ni TZ tu sajaona tokea nimezaliwa
 
Back
Top Bottom