Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Je ni vizuri kusubiri hadi wote wawili muwe katika utayari wa kuanza maisha ya ndoa na mkubaliane au ni vizuri kulazimishana kwamba "ni lazima unioe au tuachane"? Je ndoa ya kupeana ultimatum na mwisho mtu analazimika kupeleka washenga kwenu itakuwa ni ndoa kweli?
Lakini upande mwingine, kama dada hatamhimiza kijana amuoe si anaweza kujikuta anasubiri daima adumu? Wakioana kwa kulazimishana itakuwa ni maisha ya furaha huko mbeleni au ndiyo yatakuwa yale yale ya "isingekuwa wazazi wako mimi nisingekuoa wewe"? ..
Au zile za pressure ya wazazi kuwa "unangoja nini" mwisho mtu anaamua kujichukulia mke ili kuwatuliwa wazazi au kukubali kuchukuliwa ilimradi watu waache kusema sema...
Ndoa siyo hiari na mapatano?