Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,039
- 5,560
Tanzania hii kila uchwao ma pastor wanaibuka na kuwa wengi zaidi, wengi wakihubiri habari za Mwenyezi Mungu. Wametokea kuwashawishi watu wengi kuwafuata ama kuwa nao katika makanisa yao. Asilimia kubwa ya hao ma pastor wamekuwa na utajiri mkubwa mno kupitia makanisa yao.
Baadhi ya hao ma pastor ni kama, pastor Tony Kapola, pastor Dale, pastor Boniface Mwamposa, pastor GeorDavie na wengine wengi. Hawa ma pastor wamekuwa na umaarufu pamoja na utajiri mkubwa mno kupitia hizo shughuli zao za kichungaji. Wanaishi maisha expensive sana, kiasi kwamba unabaki unajiuliza ni u pastor tu ama kuna mambo mengine.
Napata mashaka kwa ile misafara yao ya magari ya gharama ni SADAKA pekee imefanya vile? Wanasukuma ma G Wagon, BMW, Benz za maana na nyinginezo nyingi za bei mbaya. Ni kweli Tanzania hii waumini wao wanatoa kiasi kile, inatia mashaka sana.
Inakuwa ngumu kuamini.