ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,154
- 4,184
Habari za wakati huu,
Kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusu Uraia Pacha kwa Watanzania na watu wengine ambao wanahitaji kuwa na Uraia Pacha. Hili ni swala ambalo linahitaji mjadala wa kina, lakini je, ni zipi faida za Uraia Pacha?
Mimi leo nataka nizungumzie zaidi faida za Kiuchumi.
Tukiruhusu Uraia Pacha tunarahisisha sana shughuli za kiuchumi na kibiashara. Kwa mfano kama mimi ni Mtanzania ambaye nafanya biashara na nchi kama China, badala ya kuhangaika na uombaji wa VISA kila mara ninaposafiri, basi natumia tu Passport yangu ya Uchina nakuwa naingia na kutoka China kama ninavyotaka. Yaani nikiamka asubuhi naweza kuanza safari ya kwenda china kama vile naenda Matejoo.
Masharti ambayo ninapendekeza kwa ajili ya kutoa Uraia Pacha ni kama ifuatavyo:
~ Kwa wageni wanaotaka Uraia wa Tanzania kwanza lazima wawekeze angalau Dola laki 2 hapa Tanzania katika Sekta za Kilimo, ufugaji, elimu na afya.
~ Lazima waishi Tanzania kwa angalau miezi 3 kila mwaka.
~ Lazima walipe Tozo ya kila mwaka ambayo haipungui Dola 2000, hii ni nje ya malipo ya kodi iwapo wanamiliki kampuni au biashara.
~ Lazima wawe na makazi ndani ya Jamhuri ya Tanzania.
Kwa Watanzania ambao ni wazawa Masharti yao yawe kama ifuatavyo:
Masharti ya Juu hapo yahusike pamoja na yafuatayo na;
~ Awe na repatriated income ambayo inatoka kwenye nchi ambayo anataka kuwa na uraia wa nyongeza.
~ Awe na familia ambayo inaishi Tanzania.
Masharti na taratibu zingine zinaweza kuwekwa kwa kutegemea na uzoefu wa nchi nyingine.