Asalaam Aleikum, bwana asifiwe!
Wakuu zangu nakutahadhalisheni sana na hizi habari zenu za CUF na Chadema...
Kama wewe ni mwanachama wa CUF au Chadema nakuombeni sana muachane kabisa na maswala ya dini..
Kwa taarifa za ndani nilizopata, moja ya mkakati rahisi wa CCM ambao wameuweka kiporo hadi siku maalum ni kuutangazia Umma kwamba CUF ni chama cha Waislaam na Chadema ni chama cha Wakristu - inatisha!
Maneno hayo tu yatawavuruga wananchi na CCM ataibuka mshindi pasipo kuangalia viongozi wao ktk UFISADI..
Trust me, jamani niamini ktk hili moja tu...CCM wanasubiri wakati muafaka wa kutumia dhana hiyo na hakika wananchi wengi watawakimbien,Msifanye mchezo kabisa na nguvu ya imani za watu...Acheni kubeza dini za watu, acheni kubeza makabila wala jinsia za watu.. Definition ya mtu Primitive hutokana na cultural blindness thesis kama hizi..
Please wasaidieni vyama hivi vipate kujenga demokrasia ya kweli badala ya kuvibomoa kwa maelezo yasiyojenga..