Ni nini tatizo mpaka elimu yetu inashuka

Ni nini tatizo mpaka elimu yetu inashuka

Joined
Aug 28, 2013
Posts
33
Reaction score
4
Kiukweli jamani ninaumia sana na huu mfumo wa elimu yetu maana umekuwa ukiendeshwa kiutashi wa wanasiasa, embu angalia kipindi Mungai alipokuwa waziri alifuta biashara na kuunganisha Physics with Chemistry, yaani kila waziri akija anatambulisha kitu chake, halafu swala la shule za kata hivi kweli walifanya uchunguzi yakinifu kabla ya kuanzisha kweli au tulikulupuka coz unakuta shule hazina vifaa na watoto wanakaa chini je kweli hapo tumefanikiwa? halafu swala la mtaala kuangalia maswala ya nje wakati hayomataifa hayasomi chochote kuhusu sisi y sisi tuwasome kuhusu wao? Embu jamani tufunguke kwa maoni hivi unaona nini kifanyike turejeshe hadhi ya elimu yetu maana sasa hivi mtu anamaliza chuo hawezi kuanzisha mradi wake anangojea kuajiriwa, je ndo tumelaaniwa au tumekosea wapi?
 
Because im a father of three crids and profeshenale amu politishian hevingi hevingi noleji sinsi one naitini sixty four when zimbabwe and unguja unaited
 
Tanzania haijawekeza kwenye elimu,unatarajia elimu yetu itaacha kushuka?
East Africa Tanzania ni ya mwisho kwa kutenga less tha 2% ya GDP kwenye elimu.
Burundi wametenga 3%,Uganda 4%,Rwanda 5% na Kenya 7%.
Unatarajia kuna "BIg RESULT" hapa.
Tuna haja ya kufanya mjadala mpana.
 
Back
Top Bottom