1. Neno Ughaibuni, linatokana na neno la Kiarabu (al-)Ghaib (غيب): Likimaanisha visivyo onekana au visivyo julikani/vilivyo vichikana
Mfano, mtu anataka kuelezea umbo la Mwenyezi Mungu au kuelezea jambo ambalo lipo nje ya uwezo wake kisha akaelezea kimakosa, anaambiwa kuwa hiyo kwake ni ilmu Ghaib, yaani elimu iliyofichikana kwake/kutoijua kwa hiyo kwake inakuwa ni ghaib.
Waswahili wanalitumia ili neno kuelezea nchi za mbali zisizojulikana (Kwa wakati huo wa zamani)... Amekwenda Ughaibuni... Abroad.