Ni njaa au mfumuko wa bei?

Ni njaa au mfumuko wa bei?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Serikali iliruhusu nchi za jirani kusomba vyakula toka moja kwa moja kwa wakulima na nchi kama Kenya wakawa wanasindika na kuuza nchi za vita kwa nembo yao kama vile Somalia na Sudan Kusini.

Sasa baada ya hali kuwa tete nchini (bei kubwa na uhaba), serikali sasa inazinduka usingizini na kutoa vibali chakula kiagizwe toka nje ya mipaka.

Mhe. Bashe alivyokuwa bingwa wa kupiga kelele Bungeni kabla hajawa waziri, sasa ni dhahiri amepwaya kwenye nafasi yake hiyo hivyo naye pia anastahili kupigiwa kelele.
View attachment 2520895

Kwa kweli Bashe amefeli mchana kweupe....
Bashe atoe chakula kwenye SGR awape wananchi badala ya taifa kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza chakula toka nje ya mipaka ya JMT na kama ilivyokuwa kawaida yetu wafanyabiashara wataingiza chakula kibovu, watakwepa kodi au wataomba msamaha wa kodi na nchi itakosa mapato.

Tunapotumia fedha za kigeni yafuatayo yanatimia kwenye uchumi wa taifa:-

1. Sarafu yetu inakuwa hatarini kushuka thamani kwa sababu tunatumia ela zetu nyingi kununua fedha za kigeni ambazo tukio hilo huzitengenezea uhitaji mkubwa.

2. Thamani ya sarafu ikishuka hutengeneza mahitaji ya fedha nyingi kwenye mzunguko.

3. Fedha zikiwa nyingi kwenye mzunguko husababisha mfumuko wa bei za bidhaa na huduma.

5. Uchumi huwa hatarini kuporomoka.

Awamu ya Magufuli Tz ilifanikiwa kuondoka kwenye kundi la nchi zenye njaa Afrika na kuingia kwenye kundi la mataifa yenye usalama wa chakula (Food Haven).

Wajasiriamali wengi wamefunga stoo za chakula cha jumla kwa kushindwa kumudu bei mashambani. Kitendo hiki kinaikosesha TRA mapato ya taifa.

Taifa linapokosa mapato miradi mingi hukosa kukamilika kwa wakati na kuilazimu serikali kwenda kukopa na kuzidishia taifa mzigo wa madeni.

Tumeruhusu mataifa ya jirani yamesomba chakula (akiba ya wakulima) kwa kigezo kwamba wana baa la njaa kumbe wameenda kuuzia (kwa brands zao) mataifa yaliyo vitani na kutengeneza ela za kigeni huku sisi tunatafuta ela za kigeni kuagiza chakula.

Si ajabu Wakenya wakaturudishia chakula chetu kwa kuwalipa ela za kigeni na si ajabu wafanyabiashara wetu wakaagiza toka Kenya chakula kile kile chetu.

Nadhani Mhe. Waziri Bashe MB asimchafue Mhe. Rais kwa utendaji mbovu ulioliingiza taifa kwenye mashaka ya usalama wa chakula.

Ingekuwa Mhe. Bashe ni Waziri kwa rafiki zetu China unadhani kipi kingejiri?
Screenshot_20230218-142758.jpg
 
Ingekuwa Mhe. Bashe ni Waziri kwa rafiki zetu China unadhani kipi kingejiri?View attachment 2521583
Ni kweli, maghala ya chakula yafunguliwe... Mambo ya kuagiza chakula nje siyo Jambo lenye afya kabisa
 
Back
Top Bottom