Ni njia gani naweza kuitumia kuweka Pingamizi Mahakamani?

Ni njia gani naweza kuitumia kuweka Pingamizi Mahakamani?

nkolaniwe

Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
24
Reaction score
1
Tulisomewa shitaka Mahakamani mimi na wenzangu wanne, ila mimi naona kama sihusiki. Naomba msaada ni namna gani naweza weka Pingamizi katika kesi hiyo?!
 
Mtafute mwanasheria akupe maelezo, hapa unaweza ukachelewa kupata maelezo matokeo yake ikaku-cost......Changamka jiteteee.

Pole kwa yaliyo kukuta!
 
Tulisomewa shitaka Mahakamani mimi na wenzangu wanne, ila mimi naona kama sihusiki. Naomba msaada ni namna gani naweza weka Pingamizi katika kesi hiyo?!

Japo neno shtaka huwa linaingia moja kwa moja katika kesi za jinai ni vizuri ukasema hiyo kesi yenu ilikuwa ni kesi ya aina gani na ipo katika mahakama ya ngazi gani ili iwe rahisi kusaidiwa kwa uhakika.. tuje moja kwa moja kwenye suala la msingi lililoulizwa,

Kama ni kesi ya jinai basi utapinga kwa kukana shtaka hilo pale unaposomewa na utasubiri upelelezi ukamilike na ushahidi utolewe, kama hauhusiki basi itajulikana mwisho wa kesi ambapo utaachiwa, kama unaamini umesingiziwa kabisa na aliyefungua kesi hiyo kafanya kwa makusudi kwa lengo la kukukomoa tu, pindi itakapoisha unaweza kufungua kesi ya madai kuwa umedhalilishwa (tort case) au umepotezewa muda makusudi na utadai gharama ambazo unadhani unastahili kulipwa kwa udhalilishaji uliofanyiwa au kwa muda uliopotezewa.

Kama kesi hiyo uliyosomewa shitaka ni kesi ya madai, basi kuna nyaraka (pleadings) utatakiwa kuandika na kuziwasilisha mahakamani ukipinga kushtakiwa kwa vile wewe sio mhusika katika kesi hiyo, utatakiwa kutoa sababu za kwa nini unadhani hauhusiki. Aliyekushtaki atatakiwa kujibu pingamizi hilo kwa kupinga ulichokisema akitoa sababu za kisheria zilizopelekea yeye kukushtaki. Mapingamizi kwa lugha rahisi ni sababu za kisheria zinazofanya kesi isiwe sahihi kuendelea kusikilizwa..

Lakini kama wewe sio mtaalamu wa mambo ya sheria, ni vizuri ukiwatembelea wataalamu wa sheria physically waakushauri kuhusu hilo. Mkielewana vyema wnaweza kukuandikia hata hilo pingamizi..usiogope gharama, siku zote mambo huwa yanazungumzika.
 
asante ndugu sajo kwa ushauri wako bila shaka upo sahihi.
 
Back
Top Bottom