Ni njia gani ulitumia hadi ukawa Tajiri?

hizo ni fikra potofu ndugu yangu na ukiwa na mawazo kama hayo utaendelea kuwa hivyo hivyo.kulikuwa na mtu tajiri kama mfalme suleiman? je mfalme suleiman anatabia kama ulizo ziorodhesha?
 
hizo ni fikra potofu ndugu yangu na ukiwa na mawazo kama hayo utaendelea kuwa hivyo hivyo.kulikuwa na mtu tajiri kama mfalme suleiman? je mfalme suleiman anatabia kama ulizo ziorodhesha?
hiyo ndo siri kwani usilo lijua kwenye mafanikio unatakiwa ufanye kipi
 
Mimi siyo tajiri ila mwaka huu mwanzoni nilipata bahati ya kukutana na wafanyabiashara wachache wa Tanzania wenye mafanikio ambao tunaweza kuwaita matajiri. Nilishiriki kufanya survey ya benki ya dunia kuhusu viwanda vidogo na vya kati vinavyojishughulisha na utengenezaji na uchakataji wa mazao ya chakula.

Kitu ambacho nilijifunza kipindi chote nilipokuwa karibu na matajiri hao wote, wengi ni waoga wa kutoa taarifa sahihi walifanikiwa vipi, sababu kuu ni aidha wanaigopa serikali especially TRA pia wanahisi taarifa yeyote itakayotoka kwao ni siri ya biashara (trade secret) kitu ambacho si sahihi. Majority ya hawa watu ni over 35 years old. Dah! vijana tupo nyuma sana aisee. Mwisho kabisa hawa ni watu ambao wako busy sana katika ratiba zao za kila siku, unaweza kumtafuta wiki au mwezi usipate nafasi ya kuonana nae. Naomba niandike kwa kifupi stori kama tatu za baadhi ya wafanyabiashara hawa naamini kuna kitu tunaweza tukajifunza sote kwa pamoja.

1. Stori ya kwanza ni ya mama mmoja ambae yeye ni mmiliki wa kiwanda cha kuoka mikate na vitafunwa(Bakery). Mama huyu ana umri wa miaka zaidi ya 50 kwa kukadiria, yeye alikuwa mama wa nyumbani lakini baadae alijifunza ufundi cherehani na kuanza kushona. Anasema alikuwa akishona nguo kwa muda mrefu kabla kuja kuanzisha biashara ya bakery. Anasema katika eneo lake la kazi alipokuwa anaendelea na shughuli zake za ufundi kushona kulikuwa na bakery. Anasema fremu yake ilikuwa imepakana na hiyo bakery hivyo ikawa rahisi kwake kuzoeana na baadhi ya wafanyakazi wa hiyo bakery.

Basi kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, akajikuta anatamani na yeye kuifanya ile bishara ya bakery. Tatizo likawa hajui aanzie wapi, basi ndipo alipomuuliza mmoja ya wafanyakazi wa ile bakery. Mfanyakazi yule akamwambia biashara ile ni rahisi unaweza kuanza hata ukiwa na mtaji mdogo, basi yule mama akaanza kukununua vifaa vyake vya bakery taratibu ambavyo alitumia kama miaka miwili kukamilisha set nzima ya kuanzia na vilikuwa na thamani ya almost Tsh 300,000. Basi anasema siku ya kwanza alifungua bakery yake nyumbani na alianza na mfuko mmoja tu wa Unga wa ngano akiwa na mfanyakazi mmoja tu. Then akiwa amekwisha anza ndo akaendelea na utaratibu wa kurasimisha biashara yake kwa maana ya kusajili leseni ya biashara, TFDA na BRELA.

Baada ya kuona demand ya bidhaa zake ni kubwa sana akaamua kuingia benki na kuomba mkopo wa vifaa na kuongeza uzalishaji katika kiwanda chake. Ndani ya miaka mitatu basi akawa amefanikiwa kupewa mkopo wa zaidi ya Tsh 100 milioni ambazo alipewa kama vifaa vya kutendea kazi. Kiwanda chake kilianza mwaka 2012 mwishoni akiwa na mfanyakazi mmoja lakini sasa hivi ameajiri vijana kama 20 hivi wengi wao ni kutoka VETA. Pia ameajiri mfanyakazi wa muda(part time) mkaguzi wa mahesabu ambaye anakagua pamoja na kumpa ushauri wa mambo ya kifedha katika biashara yake.

Itaendelea.....
 
mkuu fafanua hizo mil 105 umezitengenezaje mana ninafuga kwa mda mrefu ila sijawahi shika hiyo chapaa
 
Mtu kukutajia alipataje pesa inakua ngumu sana, hata wale waumin wa mzee wa upako hawasemagi kama waliiba au la, wao husema tu mwaka jana sikua na gari, sa iv nna prado.
 
Huo ni wa kishirikina ila wapo matajiri wachamungu.
Chunguza uone
 
me nafikiria hilo la uchaw tu kama lipo sio
zur hay engine ni sahihi kufanya kwa tajir
kwasabbu ni kitu kibaya kwa mtu mweny
mafanikio kuendelea kukaa na watu
wanaokaa vijiweni muda wote na watu kama
hawa kazi yao kuomba ela tu ukiwapa
mawazo hawayafanyii kazi.kuwa na marafiki
wakaa vijiweni no sababu kubwa
yakukurudusha nyuma story Zao in za
anasa tu yani wanawake tu akini wee
unasema roho mbaya
 
Utajiri unaanzia na mali kiasi gani?
Maana kuna jamaa akiwa na milioni 10 anajihesabu tajiri wakati kwa mwingine ni mshahara wa mwezi. Ni hela ya matumizi.
 
ushauri wangu kwako, mbali na kilimo pia zama ktk ufugaji hasa wa bata maji, na sungura hawa wanalipa sana, na kama upo tayari kuanza na ufugaji wa bata nipo tayari kukusaidia kwa kukupa short course ambayo ni bure kabisa.
Mkuu mi niko tayari kuanza kufuga sungura naomba nikupm
 
Kama million ngap???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…