Ni njia ipi nzuri zaidi ya kutengeneza business capital?

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,662
Wakuu ni njia ipi nzuri zaidi ya kutengeneza business capital from scratch? Yaani, kwa mfano una wazo zuri la biashara lakini huna mtaji na lengo lako ni kupata mtaji mdogo na kuukuza haraka ili uweze kufanya hiyo biashara. Assume kwamba hukopesheki bank wala hakuna mtu anaweza kukukopesha!

Ukiwa na Tshs 1 mil. cash in hand, ni biashara gani unaweza kufanya ili baada ya miaka mitatu uwe umepata maximum profit? Na hiyo income ambayo unaweza kuigenerate kwa kutumia mtaji wa 1 mil. in 3 years unadhani kwa hesabu zako itakuwa Tshs ngapi?

Nataka kupata uzoefu wa wajasiriamali mbalimbali hasa jinsi walivyocompound mitaji yao ya biashara au walivyoweza kutengeneza mitaji mikubwa ya biashara from scratch!

Unaweza kutupa uzoefu wako, ya kwamba labda mwaka fulani ulikuwa na mtaji kiasi fulani, say Tshs X, ukaanza biashara W na baada ya miaka kadhaa ukawa na mtaji mkubwa Tshs Y.

Lengo hapa ni namna gani mtu anaweza kutengeneza mtaji wa biashara au kukuza mtaji wa biashara exponentially.

NB: Mifano inayohusisha biashara haramu kama ya madawa ya kulevya na ujangili hairuhusiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…