Binafsi ninasema maneno haya yanafanana kwa sababu neno ONA limefanana sana na neno PONA kiumbo.
Kupona maana yake ni mgojwa kutoka katika ugonjwa,
Dawa anazomeza mgonjwa zinaMPONYA yaani zinamfanya aPONE,
Daktari anayempa mgonjwa dawa anamPONYESHA au anamPONESHA,
Hivyo, kuONA ni kupata taswira ya kitu kwa kutumia macho,
Macho ndiyo humfanya mtu aONE ama sema yanamuONYA,
Kitu ama hali itakayokufanya uweze kupona hukuonyesha.
Hapo mwanzo neno hili lilipoanza kutumika halikumaanisha KUONYA( kutia mtu adabu).
Kuna mtu alimkosea (alimuudhi) mwenzake, sasa kwa vile yule aliyeudhiwa hakuwenza kumuadhibu aliyemuudhi kwa wakati ule, akamwambi ngoja utaONA nitakutia adabu. Baadaye yule aliyeudhiwa akamuadhibu yule aliyemuudhi ( ili aONE kama alivyokuwa amemwambia awali, ngoja utaONA). Watu walioshuhudia akimuadhibu wakasema amemuONYA. Kuanzia wakati huo kuonya likawa linatumia kumaanisha kuONYA(Uliyokuwa ukiijua wewe, kutia mtu adabu) lakini bado neno hili ONA halijapoteza maana yake ya mwanzo.