Ni pikipiki gani nzuri kwa bodaboda?

Ni pikipiki gani nzuri kwa bodaboda?

King snr

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
1,165
Reaction score
1,470
Habari zenu wakuu,

Naomba kujua pikipiki nzuri kwa ajili ya boda boda nahitaji kununua pikipiki used nijaribu biashara ya bodaboda
 
Kila mkoa huwa na aina fulani wanayopendelea kutumia kama bodaboda mf, Moro-Haojue, Dom,Dar-Boxer, Mbeya- Kinglion so angalia na aina ya shughuli utazokuwa unafanya kama uliko kuna mizigo mikubwa ya kubeba kinglion inafaa zaidi ila pia kwa ulaji mdogo wa mafuta Haojue ziko vizuri pia ni nyepesi balaa kama unapenda mabio.
 
Habari zenu wakuu,
naomba kujua pikipiki nzuri kwa ajili ya boda boda nahitaji kununua pikipiki used nijaribu biashara ya bodaboda

Mkuu kwenye mishe ya pesa huwa hatujaribi bali tunafanya hivyo Kama unataka kujaribu basi game itakushinda.

Kama unataka kufanya boda chukua
TVs hlx 150 x mdomo wa mamba.
Kwanza ina sofa nzuri na pia ipo juu na kufanya wateja wengi kupenda kuipanda.

Mafuta unatembea 50km kwa litre
 
Mkuu kwenye mishe ya pesa huwa hatujaribi bali tunafanya hivyo Kama unataka kujaribu basi game itakushinda.

Kama unataka kufanya boda chukua
TVs hlx 150 x mdomo wa mamba.
Kwanza ina sofa nzuri na pia ipo juu na kufanya wateja wengi kupenda kuipanda.

Mafuta unatembea 50km kwa litre
vipi bei yake ikoje
 
shukrani mkuu,
kati ya boxer na Tvs ipi bei iko juu?
Kuna Tvs ambazo zina bei zaidi ya boxer na zipo ambazo ziko chini ya boxer ila boxer kwa sehemu niliyopo mil 2.4 unachukua mpyaa.
 
2680000, chombo bora ila nje ya mji sidhani kama utafurahia, huko upate t better, san lg, fekon utafurahia
San lg simshauri atakuwa analala hoi ataishia kusingizia wachawi wanamlimisha usiku.
 
bei imechangamka sana bajeti yangu ni 1M naweza pata used?
Kwa hiyo chuma alosema jamaa kwa hiyo bei blaza kupata ni ngumu na hata ukiipata lazma itakuwa ya wizi au ina historia ya ajali na inatafuta pakufia maana hazina muda sana sokoni.
 
Usajili ilikuwa gharama iliyoko kwenye bei ya pikipiki ila bima sikukata mkuu japo palepale pembeni ya ofisi yake kuna ofisi ya bima.
 
Back
Top Bottom