Ni pombe gani huwa inakupa mzuka na kuona Dunia ni sehemu salama?

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,093
Kwa kweli Pombe ina ka-vibe kake fulani hasa ukiwa na washikaji au Mbebezi wako halafu mkatoka na usiwe na pesa ya mawazo. Yaani piga kilaji, piga nyama, huku ukiwa na uhakika wa usafiri wa kukupeleka sehemu ya kupumzika.

Binafsi nikifika sehemu ya monde halafu nikaanza kula Windhoek zangu baridi huku Muziki unagonga masikio Yangu, nasahau tabu na karaha zote za dunia. Halafu nione na totoz kali zikipita basi mimi burudaaaani kabisa.

Kwa upande wako ni kilaji gani huwa unakipenda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…