Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kwa kawaida hawa watekaji na wauaji wanapofanya uharamia kama waliomfanyia Ali Kibao RIP, huwa wana watu wao ambao huwa wamewapanga barabara zote watakazopita ili wasipate kizuizi mahali popote wakiwa na mateka. Hata wasipokuwa na mateka, wakishafanya tu uharamia, huwa hawataki wasimamishwe mahali popote pale hata kama kuna kizuizi cha polisi, wasije wakaojulikana kwa wananchi wa kawaida.
Hivyo, siku hiyo wanayofanya uharamia, barabara zote, hasa maeneo yanayokaribia eneo wanaloenda kufanya uharamia, kuanzia walipo traffic police, mpaka polisi wa kawaida, huwa wanakuwa na mtu wao.
Tumeambiwa kuwa watekaji walikuwa na magari mawili, yote yakiwa hayana plate numbers, hii ina maana wakipita eneo lolote lile lenye askari, kama si miongoni mwa hao watekaji, wangesimamishwa.
Lakini kwa sababu barabarani na kwenye vizuizi vyote huwa wamewaweka watu wao, wanapita bila kusimamishwa wala kuhojiwa; tena kukiwa na msongamano wa magari au taa za barabarani zikiwa nyekundu, wao wataruhusiwa kupita kwa kusaidiwa na askari wa usalama barabarani.
Hata walipofanya shambulizi dhidi ya Lisu, mara baada ya shambulio, mashuhuda wanasema, askari wa barabarani, walisimamisha magari na bodaboda ili gari lile lililokuwa na washambuliaji lipite bila ya kizuizi chochote.
Kama kweli mamlaka za juu za uongozi wa Serikali hazikuhusika, iwe ni moja kwa moja au kwa maelekezo ya jumla, kwenye uovu huu, haiwezi kupita hata siku 2 wahusika wote watajulikana.
Wakiwakamata askari wa barabarani waliokuwepo siku hiyo, barabara zote zinazoelekea na kutoka Tegeta, mara moja wahusika watapatikana.
Maana wanachofanya hawa watekaji, siyo kwamba siku hiyo ya uharamia wataongoza magari yote, bali wanaenda eneo ambalo wapo askari wa kawaida, anabakia pale huyo miongoni mwa hao watekaji, wale askari wa kawaida wana-mute.
Yule aliye sehemu ya watekaji ndiye anatoa maelekezo kwa askari wa kawaida. Na gari la watekaji likishapita, naye ataondoka.
Bahati mbaya Rais ameomba apelekewe taarifa baada ya uchunguzi, hakuagiza wahusika wakamatwe mara moja. Angeagiza kuwa wahusika wakamatwe mara moha, mpaka muda huu, tayari kuna watu wangekuwa wamekamatwa.
Nakumbuka wakati wa uongozi wa Mkapa, kuna mauaji yalifanyika kwenye mgodi mmojawapo wa wazungu. Mkapa aliagiza kuwa anataka wahusika wote wakamatwe mara moja. Ingawa polisi hawakuwepo kwenye tukio wajati uovu unatendeka, ndani ya siku 1, watu kadhaa walikuwa wamekamatwa, na baada ya siku 3, mhusika mkuu katika kupanga uvamizi ule alikuwa amekamatwa.
Halikadhalika, wakati wa mauaji ya RPC wa Mwanza, Rais alitoa amri kuwa wahusika wote lazima wapatikane. Ndani ya wiki 1, wote walikuwa wamepatikana.
Hata katika hili, Rais angekuwa ametoa amri kuwa anataka mara moja wahusika wakamatwe, sahizi kungekuwa tayari kuna orodha ndefu ya wahusika, wakiwa tayari wamekamatwa.
Polisi wetu siyo kwamba hawana uwezo bali uwezo wao unafifishwa na kuharibiwa na wanaowaamuru.
Ukitaka kuujua uwezo wa polisi wetu, mtu yeyote yule, hata kwa kificho kikubwa, aue kamanda wa polisi, hata kwa kificho kabisa, nakuhakikishia muuaji atakamatwa tu, hata kama mauaji yamefanyika kwa kificho kiasi gani.