kitalolo
JF-Expert Member
- Dec 4, 2006
- 1,827
- 708
Nimesikia kuwa ikiwa ulioa mwanamke na ukamkuta tuseme ni mdada tu wa nyumbani hana kazi na elimu yake ni yawaida ikatokea baada ya kuwa kwenye mahusiano au ndoa ukaamua kuendeleza kielimu pengine hata kumwezesha kupata kazi eti wazee wanasema kuna uwezekano mkubwa wa demu huyo kuachana na wewe kwavile pengine mlipoazna mahusiano aliona kutokana na levo yake wewe ndio unayemstahili sasa akipanda chata atataka kuwa na wa levo ya juu zaidi kwahiyo uwezekano wa yeye kutoka nje ya ndoa unakuwa mkubwa zaidi au hata kuachana maana sasa anakuona kama vile uko matawi ya chini na yeye yuko matawi ya juu. pia kuna usemi kuwa mwanamke ataona kuwa kwavile wewe umeamua kumwendeleza kielimu ni sawa na unamdhgarau na unamwona kama sio msomi au humpendi tena mbaya zaidi ni wanasema ni wakati wa kumtongoza demu au wakati wa uchumba ukamwahidi vitu kama kusomeswa na mengineyo kama hayo eti anaweza kukubali au kuingia kwenye ndoa kwavile tu anajua atasomeshwa na mambo mengine kama hayo. je kuna ukweli wowote katika hili na kama ni kweli je nini kafanyike?