Ni rahisi mwanamke kukuacha ikiwa>.......

Ni kweli uwezekano ni mkubwa zaidi...... Muhimu omba MUNGU usiachwe baada ya kumsomesha...
 
kwani we unaoa kwa kumsomesha au kwa kuwa unampenda?Pili anakubali uoane nae ili umpeleke class au kwa kuwa anakupenda? kwa 7bu zozote nje na upendo, kwa vovote vile hiyo ndoa ingevunjika tu.Mi naamini kwa mwanamke mwenye mapenzi ya dhati na wewe ukifanya kitendo cha busara hivo ndo atakupenda milele.
 
mmh haya mambo magumu jamani
kuna uwezekano akawa nawe maisha yake yote
ila pia kuna uwezekano asiwe nawe
sababu
mtu unaweza kuwa unamsoesha mtu ndio..
ila sas kuna tabia ambazo yeye hazipendi kutoka kwako
na amekuvumilia au ameshakueleza mara kadhaa ila haubadiliki
japo unamsomesha sawa...sasa yeye aolewe tu nawewe
at the time kuna vitu anajua wazi vitamuumiza maishani?

maana tusilaumu tu upande wa pili wa mwanadada kumuacha mwanakaka
inawezekana tatizo lipo kwa kaka na hataki kubadilika
isitoshe wakati huo mwanadada amesha pata exposer so anaelewa nini maana ya mapenzi na nini haki zake ndani ya ndoa so anao
uwezo mkubwa wa kufanya best selection
so msomeshe tu ila hope for the better....
 

usijali mkuu kama wa kuachika utaachika tu na tabia za wanawake mkuu si unazijua? Hata wanaume wengine akikutana na ajiri mwanamke akimuweka ktk matawi ya juu wengi hukimbia kitu ambacho ni Upuuzi tu...
 
Je akijisomesha mwenyewe kwa vihela vyake huku akiwa ndani ya ndoa, napo huwa wanabadilika?
 
Ukiwa na mambo ya kike lazima upigwe chini teh!
 
Mkuu kwanza umenichosha sana coz nimesoma bila kupumzika. Pili ulichoongea ni CRAP...
 
Nitamsomesha mwanamke baada ya kuzaa naye, kwan hata akiniacha naamin mtoto atanufaika na elimu ya mamake niloigaramia!
 
Ukweli ni kwamba, zaidi ya asilimia 95 ya wanaume walo-attempt kuwasomesha wapenzi wao waliishia kupigwa kibuti mwisho wa siku. Sasa kama na wewe unataka ku-prove hilo, jaribu. Nadhani haitokuathiri sana kwa kuwa unafahamu nini kitaweza kutokea hapo baadaye.
 

Wanawake wanaofanya hivyo ndio Vitalolo hasa, tena vya leshuu!
 
next tym omba ushauri kabla..kwasasa huna namna we muendeleze tu kielimu..Kama anasoma mbali nawe, jitahidi kuwa makini na ujio wa kushtukiza maana waweza bebeshwa mimba isiyo yko.
 
Kuna tofauti kati ya mpenzi na mke. Usilogwe kuingia kichwa kichwa kusomesha girlfriend ninakuhakikishia lazima atakuacha chance ni kubwa kwani vyuoni vishawishi ni vingi na yawezekana ajakomaa kiakili na akikomaa akiwa college anagundua wewe si choice.

Kuhusu mke nakushauri umsomeshe haraka sana. Kaka yangu alioa girlfriend wake wa miaka mingi mdada anatoka familia bora iila aliishia form four tu. Siyo siri ndugu zake japo hatukumwambia tulikuwa disappointed knowing that life is real hard ukioa mama wa nyumbani itokee unaaga dunia nani atalea watoto? Lakini to our suprise kaka soon baada ya kumuoa huyo dada kampeleka college kuchukua diploma, na sasa ana degree na ana kazi nzuri na pesa labda zaidi ya kaka na ni mwanamke mvumilivu sana maana kaka kidogo hajatulia.

Mimi kama mwanamke sidhani kama kuna mwanamke anaweza kumkimbia mumewe eti kisa amemsomesha. Sisi wanawake tunaweka familia mbele hata maswala ya kuwa ma mahusiano huku mumeo anakusomesha ni very rare; na ukiona mdada wa tabia hiyo jua hata usingemsomesha angetembea na wauza bucha tu. Kwa hiyo kaka na wengine wasomesheni wake zenu ni kama bima kwa familia.
 

ushauri mzuri asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…