Ni Rasmi sasa kiwanda cha magari ya Volkswagen chafunguliwa Kenya

Ni Rasmi sasa kiwanda cha magari ya Volkswagen chafunguliwa Kenya

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
"Baada ya zaidi ya miaka 60 ya kuunda magari ya Volkswagen kwenye mataifa ya kaskazini na kusini mwa Afrika, leo nafurahi kwamba tumepiga hatua hii ya maendeleo nchini Kenya," alisema Dk. Diess wakati wa ufunguzi wa kiwanda hicho nje kidogo ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Rais Kenyatta ameuita uzinduzi huu kuwa ni "ndoto iliyokuwa kweli", akisema kwamba ni ushahidi wa mashirikiano kati ya serikali yake na sekta ya viwanda na hatua kuwa ya kuielekeza Kenya kwenye kuwa taifa la kiviwanda.

Kenyatta ameipongeza serikali ya Ujerumani, Kampuni ya Volkswagen Group na wawekezaji kutoka Ujerumani ambao wameahidi sio tu kutoa mafunzo kwa wafanyakazi katika Kiwanda cha Kuunda Magari cha Kenya Vehicle Manufacturers, bali pia kuijengea uwezo sekta nzima ya uundaji magari.

Gari la kwanza aina ya Volswagen Vivo limeshuhudiwa kukamilika kuundwa katika kiwanda hicho. Diess amempongeza Rais Kenyatta kwa kujitolea kwake kuhakikisha mradi huo umefaulu.

Gari muundo wa VW Polo Vivo ambayo inatengenezwa sasa nchini Kenya kwenye kiwanda cha Volkswagen.

"Ningependa kumshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kusimama na mradi huu. Kuanzia mkutano wetu mjini Berlin hadi kutiwa saini kwa mwafaka wa makubaliano wewe Mheshimiwa Rais ulionyesha kujitolea kwako kwa kujiandaa kufanya mikutano ya mara kwa mara licha ya shughuli zako nyingi."

Rais Kenyatta ameahidi kwamba serikali kuu na serikali za kaunti zitanunua magari kutoka kiwanda hicho kipya ili kuimarisha biashara.

Kampuni ya Volkswagen itaanzisha tena utengenezaji wa magari nchini Kenya ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na inatarajia kuuza magari zaidi katika mataifa ya Afrika Mashariki.

"Baada ya kusitisha kwa muda wa miongo minne uzalishaji wa magari nchini Kenya, Volkswagen itatengeneza magari modeli ya Vivo", walisema Rais Kenyatta na mkuu Volkswagen nchini Afrika Kusini, Thomas Schaefer.

Kampuni ya magari ya Volkswagen inashirikiana na kampuni ya DT Dobbie inayouza na kutengeneza magari ya aina ya Volkswagen nchini Kenya.

1482342892617.png
 
Kenya kuna soko/market threshold ya magari mapya kwa sababu kuna sera, sheria na mipango inayotaka na kuratibu watumishi wa umma na makampuni binafsi kununua magari mapya, siyo mitumba. Hii ni tofauti na Tanzania ambapo watumishi wa umma na makampuni binafsi hununua mitumba badala ya magari mapya. Mikopo ya kununua magari mapya hudhaminiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii (hakuna pato la kujitoa huko). Wafanyakazi (vyama vyao) wa hapa nchini wanapaswa kuacha kudai pato la kujitoa badala yake wadai mifuko ya hifadhi ya jamii iwadhamini kupata manufaa ya mikopo kwa ajili ya matakwa ya maisha bora (mikopo ya nyumba na makazi, magari mapya, elimu na matakwa mengine ya watu wa daraja la kati (middle class people).
 
Viwanda vyetu, vinajitosheleza kwa mahitaji ya ndani

Serikali Hayo magari yapigwe marufuku kuingizwa Tanzania ili turuhusu viwanda vyetu vizalishe magari mengi zaidi kwa ajili ya ku export nchi kama Australia, Marekani, Uchina na mabara ya Asia

Maana bara la Amerca ya kusini, Ulaya tulisha teka soko
 
Kumbe Mzee kinyatta alienda mpaka Berlin kusotea utiaji sahii huo mradi. Hongera zake kwa kutoa kuonana na watu wa nje ya afrika
 
Sie tunahangaika na kina maxence,ben saanane,lema na faru john huku majirani zetu wakijenga viwanda tunavyoviimba.
 
Back
Top Bottom