Ni sababu ipi mtu huitwa marehemu na mwingine kuitwa hayati?

Naona mara nyingi linatumika Kwa watu walikuwa na michango fulani ktk jamii
 
Umeeleza vyema.
Naomba niongeze neno jengine unisaidie maana yake "Buriani". Maana nalo limekuwa likitumika kwa mtu aliyeaga dunia.
Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mara nyingi linatumika Kwa watu walikuwa na michango fulani ktk jamii
Sasa kwanini liwe kwetu tu kwa maana tofauti?
Sidhani kama kuna neno linafanana na hilo kwa kizungu (kwa mfano)
Ambapo heshima ya au mchango katika jamii akapewa neno tofauti na LATE

Sent from my SM using Tapatalk
 
Naona mara nyingi linatumika Kwa watu walikuwa na michango fulani ktk jamii
Mkuu,
Asante kwa mchango wako.
Hayati Mwl Nyerere, Marehemu Komba utafauti huu unaletwa na nini na wote hawa kuna mchango walichangia katika jamii?
Na hii inaonekana iko kwetu waarabu kama alivyosema mwana jamvi mmoja wenzetu wazungu wanae "The Late" tuhakuna mambo mengi.
Tutafakari zaidi sababu za utofauti huu.
 
Cute wetu,
Yupo Hayati Mwl Nyerere na Marehemu Capt John Komba unasemaje hapo
 
Hayati ni yule mtu maarufu kisiasa hasa ngazi za urais na uwaziri mkuu au katika kanisa Papa na kardinali marehemu ndio akina sie
Mkuu,
Yupo Marehemu Cardinal Rugambwa mbona hatumtangulizii Hayati huyu?
 
Kufa (kufariki/kuaga dunia) it is a natural death... Hutokea kwa umri kuwa mkubwa sana au ugonjwa..nk
Kuuwawa its murder.... Hutokea kwa nafsi nyingine kushiriki katika kifo chako.... mfano kupigwa,kulishwa sumu nk... so you may see the differences
Je mleta mada unajua tofauti ya kufa na kuuawa?
Utasikia marehemu hakufa aliuawa!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…