Kumekuwa na wimbi kubwa la watu hasa wale wapenzi wa zamani wa muziki wa dansi kujiita wachambuzi wa muziki hadi kufikia kuwashawishi wamiliki au viongozi wa Redio hasa zile za binafsi kuwaajiri wakiamini watakuwa kivutio na ushawishi kwa wasikilizaji.
Lakini kiuhalisia hawa watu hawana ujuzi wowote wa muziki zaidi ya kuwa wapenzi wa bendi za zamani na nyimbo za zamani.
Hivyo wakati huo walikuwa wahudhuriaji wakubwa wa maonesho hadi kufikia hatua ya kujuana na wanamuziki wa bendi hizo na kuzikariri nyimbo nyingi na wengine walikuwa madereva taxi wakipeleka wapenzi dansini na wao kupata ofa ya kuingia bure ukumbini.
Lakini kiukweli hawana taaluma ya muziki hivyo wengi wao wakiwa kwenye kipindi huishia kupiga mastory ya matukio yaliyokuwa yakijiri wakati huo.
Sasa je ni sahihi watu hao kujiita wachambuzi wa muziki? na wengine kujipa vyeo kabisa utasikia mtu anajiita yeye ni rais wa wachambuzi wa muziki wa dansi.