Ni sahihi kigezo cha kusoma private schools hasa za gharama kutumika katika kutoa mikopo ya bodi ?

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,193
Reaction score
810
Kumekuwa na utaratibu wa bodi ya mikopo kutumia kigezo cha mwanafunzi ambaye amesoma shule za private kukosa sifa ya kupata mkopo wa bodi kwa ajili ya High learning Institution. Mimi napingana na dhana hii kwa sababu zifuatazo Mosi. Kwanza kumpeleka mtoto shule ya private sio kuwa mzazi ana uwezo kifedha, maana wengi wetu tunateseka na mikopo angalau mtoto apate msingi wa elimu bora. Ni wazi kuwa kiwango cha elimu cha shule nyingi za serikali ni duni hivyo kulazimika baadhi ya wazazi kutafuta njia mbadala. Pili. ikumbukwe kuwa mpaka mtoto anafika muda wa kwenda chuo, jua pia mzazi vyanzo vya mapato hasa kwa wafanyakazi vyaweza kuwa vimeisha, mfano kukaribia kustaafu, hivyo ni wakati wa serikali kumpokea mzazi kwani alimsomesha kwa gharama si kwa faida binafsi bali awe msaada kwa Taifa Zima. Tatu ni jukumu la serikali kuhakikisha watu wanapata elimu bora, hivyo kumnyima mkopo ni sawa na kumwadhibu badala ya kumshukuru mzazi kwa kuisaidia serikali maana kama watoto woote ambao wako private wakirudishwa shule za serikali ni wazi kuwa itakuwa balaa tupu maana wasingetosha katika majengo machache na duni yaliyopo. Ukitaka kutenda haki ni lazima ujiridhishe kuwa mzazi bado anao uwezo uleule, hana majumu mengine ya kusomesha, hana project kubwa inayotumia kipato chake kama vile ujenzi, ugonjwa n.k
 



Ni sahihi kabisa kwa hoja zako nzito.Wahusika wanatakiwa kuzifanyia kazi hoja hizi ninaamini wanapita JF.
 
uko sahihi,ila kumbuka kuwa hii nchi ni mpaka tupigane kwanza,then tutaeshimiana,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Kwanza nakubaliana na mleta mada kuwa ni haki ya kila mwanafunzi kupata mkopo. Lakini kwa sasa bodi haina uwezo wa kumpa kila 1 mkopo kutokana na vyanzo vyake duni. Ktk mazingira hayo mikopo inatolewa kwa wanaoitaji zaidi. Kufanya hivyo ilibidi bodi watengeneze jinsi ya kupima uwezo ndio wakaja na means test yenye vigezo k1wapo ni kusoma shule ya kulipia ktk elimu ya chini. Of which its very fair kwamba kama uliweza kusoma private school wazazi wako walikua na means kwahiyo it is assumed kuwa wataweza kukulipia na chuo. Ikumbukwe kuwa kuna vigezo zaidi ya kusoma private ikiwa ni pa1 na kuwa na wazazi wote 2, kazi za wazazi n.k.
 
Umeongea kwa hisia kali sana mkuu. Jambo jingine la kujiuliza ni kuwa, je elimu yetu ya vyuo vikuu, hivyo vinavyoishi kwa mikopo ya bodi kwa sasa nayo ni bora?
 
mada imenigusa,,,. Mtu form four umepiga division four ya 26 au 27 ila una credit 3 unakosa nafas ya kuchaguliwa government mzaz anajipigapiga na kuuza cha kuuza unaenda private.
 
Umeongea kwa hisia kali sana mkuu. Jambo jingine la kujiuliza ni kuwa, je elimu yetu ya vyuo vikuu, hivyo vinavyoishi kwa mikopo ya bodi kwa sasa nayo ni bora?

hiyo nayo ni hoja ya kujiuliza
 
Umeongea kwa hisia kali sana mkuu. Jambo jingine la kujiuliza ni kuwa, je elimu yetu ya vyuo vikuu, hivyo vinavyoishi kwa mikopo ya bodi kwa sasa nayo ni bora?

vyuo vikuu vingine naona selikali ingevifunga tu.
 

Sio sahihi hata kidogo, mimi binafsi nilisoma private schools kuanzia pre-form 1 hadi form 6.Lakini kote huko nilifadhiliwa na hawa watu weupe (nawashukuru sana). Kama nisingepata huo ufadhili, sijui leo ningekuwa wapi.

Cha kushangaza nilipotata kujiunga na chuo ndo hizi taarifa za ajbu wakaanza kuzileta, ilinifanya nikae nyumbani mwaka mzim. Sitaki hata kukumbuka... Namshukuru Mungu kwasasa nipo chuo, na mkopo juu (Hata hivyo nilipangwa priority program).
 
kupata mkopo ni 'undefined' ,michezo mingi ina chezeka baina ya bodi na wadau flani flani!
 
uko sahihi,ila kumbuka kuwa hii nchi ni mpaka tupigane kwanza,then tutaeshimiana,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mdau yuko sahihi, lakini kwa hili la kupigana kwakweli hapana, tena tuache hizi habari kabisaaa, jaribu kutazama majirani zetu tu hapo namna walivyopata tabu, tazama nchi ambazo zipo katika mapigano ni faida zipi zinapatikana zaidi ya kina mama na watoto ambao hawana hatia kupata dhiki na kuuawa?

Mimi binafsi siungani na wewe katika hili la kupigana.

Mungu Ibariki Tanzania, Upendo na Amani vitawale, chuki ituepuke, amen.
 
Ambacho aio sawa sasa hapo ni kipi? Sababu wewe kusomeshwa na watu weupe inahusika nini anapoongelea mzazi kutumia mkopo kusomesha mwanafunzi private? Duh, em think kabla ya kuandika bna, unaanza na hayuko sawa huku kinachofata chote unaungana na anachosema..
 
Kuna njia halali za kudai haki bila kupigana, tatizo la Tanzania hata mkiandamana kwa amani bila kufanya fujo, Polisi wakifika wanaanza kipigo badala ya kulinda tu amani na kusikiliza wananchi wanasemaje, waanzilishi wa ugomvi bongo ni serikali sio wananchi.. Mjinga anakuja na kusema "na wapigwe tu" hivi amnesty international imelala au ni wabongo wamelala? We need peace ila tutafanyeje, ukaaji kimya ndio unafanya wajione wana nguvu zaidi wanaendelea kuweka hela mfukoni, these guys are rich bna, ni zaidi ya unavofikiria, they got great houses, big cars nje ya nchi, n they keep lots of money, we mshahara rais wa bongo anataka amfukuzie Obama wapi na wapi? compare all american states zaidi ya 50 na mbongo anayerun sawa na state moja tu afu mishahara ikaribiane does t make sense?
 
if you need loan you should select priority program iwapo nao huwa wanakosa but just think globally ktk hili this year many people who have studied private schools they got loan mengine n maneno 2 but accountability is nothing,,,,,serikal vs wazazi vs wanafunzi should negotiate 2 each other so as 2 improve and supporting a student for his/her studies,,not otherwise
 
Inawezekana kabisa elimu yako ni standard seven,,,maana sitegemee mtu mwenye elimu zaidi ya kidato cha nne,,anaweza kuwa na upungufu wa ufikili kiasi hicho!nikuulize swali,,,unajua bodi ya mikopo wanafanya ujinga sana,,chuu kikuu dsm,,kuna vijana watatu ninaowajua mim wanasoma UDBS,,biashara,,wazazi wao ni vigogo serikalini,,na bado wote akuna aliyepata mkopo chini ya asilimia 80.....!wote ni zaidi ya 80,,,sasa kuna watu wanasoma uwalimu,,ambayo ni priority kwa mujibu wa serikali,,wamesoma private advance,,watoto wa wakulima,,,mkulima ameuza ng'ombe zake zote kumsomesha mtoto private,,amefaulu,,,alufu unamnyima mkopo kisa kasoma private,,na unampa mkopo mtoto wa kigogo serikalini,,kisa mwanao kasoma government school.una akili,,matope!JIPIME MWENYEWE,,,,akuna cha vigezo ni ukilitimba tu,,,wewe erg,,,,elewa mambo bhana,,nenda pale bodi ukaone magari yanayopaki pale,,,ni atari,,awa guys wana ela bhana,,,
 

sasa tutaendelea kuishi nchi mmoja,,alafu tuko tofauti mpaka lini? Mimi nakuambia kuwa ipo siku wanaovumilia watachoka,,,na hapo ndio kitakaponuka,,,sasa mimi mtoto wa mkulima nanyimwa fursa ya kusoma,,,alafu watoto wa vigogo wanasoma ili waendelee kututawala hapo baadae,,,serikali inatengeneza bomu la atari sana,,,
 

your hopeless ,,,,guy,,,,!soma majbu yako chini hapo,,,
 
aisee MKUU NI KWELI KABISA ,ALAFU MDA MWINGINE UTAKUTA MTU KASOMA PRIVATE KWA AJILI YA UFADHILI KUTOKA KWA MJOMBA ,SHANGAZI AU HATA MTU BAKI TU ILI AWEZE PATA ELIMU BORA. KUNA WATU PIA WAMESOMA GOVERMENT LAKINI UWEZO KWAO UPO KULIKO KWA YULE ALIEJIKAKAMUA KUSOMA PRIVATE .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…