Ni sahihi Kulazimishwa kuchanja chanjo ya korona?

Ni sahihi Kulazimishwa kuchanja chanjo ya korona?

Sokulu Mkombe

Senior Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
126
Reaction score
167
Habari wanajukwaa,

Nakuja kwenu wanajamvi kuuliza kama ni sahihi mtu kulazimishwa kuchanjwa hasa hii chanjo ya korona. Nijuavyo mimi mtu anatakiwa aelimishwe kisha ahiari pasipo shuruti.
Lakini Hali ni tofauti mkoani RUKWA wilaya ya NKASI kwani kinachoendelea sio uelimishaji wala uhamasishaji bali ni shuruti, nitatoa mifano kadhaa

1. Wanufaika wa mpango wa kuinua kaya maskini (TASAF) hawakuruhusiwa kusaini fomu zao ili kuchukua pesa zao kama hawajachanja korona
2. Wamama wanapoenda kliniki kujua maendeleo ya watoto wao kama ilivyo kawaida wanatishiwa kutopewa huduma kama wasipo chanja korona
3. Ndugu wa wagonjwa wanazuiliwa kuwaona wagonjwa wao kama hawaja chanja korona
4. Watu wanafuatwa nyumbani au kwenye vikundi vya vikoba kulazimishwa kuchanja

Swali langu kwenu wanajamii na Wizara ya afya je, ni sahihi kutumia nguvu kubwa kiasi hiki? Ukizingatia kuchanja ni hiari na nini kiko nyuma yake?.

Baada ya watu kuchanja wanapata shida mbalimbali za kiafya ikiwemo kupata homa kali

Wahudumu wa afya wilaya ya NKASI hamuoni kama mnatukosea watanzania?
Tumeambiwa kuchanja ni hiari kwa mujibu wa wizara ya afya ila hiki kinachoendelea hamtutendei haki kabisa.


Natanguliza shukrani
 
Mdogo wangu ukiwa maskini Huna uchaguzi. Elewa tu hii kauli uishi Kwa amani

Unajua Tasaf ni Hela za misaada Toka nje? Sasa Hela zao unazitaka ila chanjo Yao hutaki? Kama hutaki mambo yawe mengi susia chanjo zao na Hela zao/misaada Yao mingine
 
Mdogo wangu ukiwa maskini Huna uchaguzi. Elewa tu hii kauli uishi Kwa amani

Unajua Tasaf ni Hela za misaada Toka nje? Sasa Hela zao unazitaka ila chanjo Yao hutaki? Kama hutaki mambo yawe mengi susia chanjo zao na Hela zao/misaada Yao mingine
Sawa nimekuelewa ila hili la kunyimwa huduma muhimu kisa hujachanja sio sawa
 
Back
Top Bottom