Kila anayechumbia anakuwa na malengo na mipango yake na sifa alizojiwekea kuwa lazima nioe au nioelewe na mtu mwenye sifa kadhaa!!
Je unaweza kumuacha mtu wako kisa maneno ya wanaosema hata kama amekidhi vigezo vyako?
Mfano wakwambie
Ni mwizi
Ni malaya
Ana mtoto usioe mwenye mtoto
Kwao wanafiki
Au wachawi
Je utamuacha!!!
Je ipo nafasi ya washauri kwenye maamuzi yako ya mpenzi umpendaye?
Watu tunashindwa kuelewa kuwa sio eti kwa kuwa ni mshauri basi akushauri kila kitu.
Kwanza kabisa ukiona mtu anakushauri kuoa na wewe ukaoa basi ujue umeoa kwa sababu ya mshauri wako yuko tayari wewe uoe na sio unaoa kwa sababu uko tayari wewe kuoa.
Sasa kuoa unatakiwa wewe mwenyewe ndo ujishauri na uone kuwa upo tayari.suala a kutaka kuoa halina ushauri.
Pili suala la mwanamke wa kuoa hutakiwi kupata ushauri wa yeyote.
Unachotakiwa kupata ni data za huyo mwanamke wako mtarajiwa kama ana tabia njema ama hana na sio vinginevyo.
Sio kuwa eti ana sifa uzitakazo ila watu wanakuambia usioe kwa sababu wao hawajampenda,kwani wewe ndugu zako wote waliooa wanawake zao ukiwaangalia alafu imagine wewe ndo ungekuwa unawachagulia wake je ungewachagulia wake hao waliokuwa nao ?
Lakini unaishi nao hao wake zao na hamna shida aliyempenda ni mume.
Nafasi ya washauri ni kukuhabarisha mwenendo wa binti kama ana sifa anazotaka,mbali na hapo labda wakuambie kuwa kwa sasa usioe kwa sababu ya kadhaa wa kadhaa.
Laikini uko tayari kuoa eti unaambiwa huyu usimuoe eboh.
Hao washauri wataondoka utabaki wewe na mkeo.
Nyie ndo mnatakiwa mpendane kwanza.