Wadau labda kwa kuwa mimi si mpenzi wa mpira wa miguu kivile, nashangaa kuwakuta vijana wenzangu wakibishana kwa kauli kama hii, "nakufunga leo huniambii kitu mimi" huku timu anayoitetea hana hisa wala ubia nayo , hana kadi ya uanachama, hajawahi kumwona live hata mchezaji mmoja licha ya kwenye video na magazetini ,timu iko nchi za wazungu ambao wengi wanatuona kama unshapped mind persons sisi weusi, yeye si kocha mkuu wa timu, si mhasibu wa timu, si mfadhili wa timu ,si mpishi wa timu ,yaani hana nafasi yoyote katika timu husika.
Is this right?