Ni sahihi kwa mama mjamzito kubagua vyakula?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Huyu dada tangu amepata ujauzito wangu, amekuwa ni mtu wa kubagua vyakula; hataki kula mchicha, chainizi, tembele, bamia, nyanya chungu, yaani mboga za kuota shambani hataki.

Yeye anataka kitimoto, nyama ya mbuzi, kuku, samaki sato; kwa ujumla anataka kula vizuri vizuri tu, mbaya zaidi anataka ambavyo vimepikwa tayari, yeye hayuko tayari kuingia jikoni.

Amenipigia simu mara kadhaa, sipokei na amenitumia ujumbe sijajibu; naona anataka anifanye mimi mtumwa sasa.

Badala ale mboga za majani apate afya, yeye hataki; anataka kunikomoa.

Sasa wakuu, ni sahihi kwa mama mjamzito kubagua vyakula?​
 
Mwanamke anapokuwa mjamzito kuna mabadiliko mengi hutokea mwilini mwake kutokana na mimba yenyewe.

Mabadiliko hayo hutokana na homoni nyingi kubadilika mwilini mwake ili kukaribisha na kukuza kiumbe tumboni mwake.

Mabadiliko hayo huathiri hisia, afya ya mwili na akili kwa kiasi fulani na tabia ya mama na zinaweza kuwa tofauti kutoka mimba moja hadi nyingine. Kwa mfano wanawake wengi hupata kichefuchefu cha mara kwa mara na hata kutapika sana hasa mimba inapokuwa changa. Wengine hupendelea aina fulani ya vyakula, hali ya hewa, kukaa na watu fulani, mazingira tulivu au ya kelele sana nk.

Hata hivyo, mabadiliko hayo hupungua na pengine kuisha kabisa kadri mimba inavyokua. Mabadiliko hayo huwa na ya muda mfupi (miezi fulani ya ujauzito) mfano kichefuchefu na kutapika huwa kikali sana kwenye miezi ya mwanzo ya ujauzito lakini hupungua baadaye.

Kwa hiyo ni muhimu kushirikiana na mwenzako kulea mimba kwa kadri ya uwezo wenu na si kwa kukomoana kwa namna yoyote ile.
Kila la heri!
 
Sawa mkuu, ila mfuko unatoboka sana
 
Mchicha mboga ya nyongeza Baba kijacho 😀😀😀😀😀
Alipokuwa anamwagia ndani kijacho alistarehe Sana expectant father saivi yamegeuka kuwa stress komaaa kuzaa mtoto kuna stage nyingi sana😄😄😄😄😄
 
Back
Top Bottom