Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Wasalaam wakuu, tafadhali naomba kufahamu kutoka kwa wataalam kama kweli ni sahihi au si sahihi kwa mtu mwenye uzito ulizidi na mwenye uhitaji wa kupungua uzito kama itakuwa sahihi kwake kutumia maziwa ya ng'ombe mara kwa mara. Asanteni.
KWANZA unatakiwa ujue wewe kama wewe nini kilichokuletea unene
-mazoezi
-kula vibaya
-kuridhika
-homoni kukaa vibaya hasa insulini
PILI uanze kupambana na nini cha kufanya
TATU fahamu ya kuwa maziwa yana kiasi gani cha wanga, mafuta na protein na kisha jiulize kiasi hicho kinaweza kukuletea au kukuongezea kilo ngapi kwa siku.
Karibu tena kama una la kufunguka zaidi
Piga tizi, usipende kula vyakula vyenye mafuta na jitahidi kunywa maji mengi
Najitahidi kufanya hivyo Mkuu, ila tatizo linakuja kwenye mlo. Nataka kupiga chini mlo wa usiku kabisa ili niwe napiga glass ya maziwa fresh tu
Mkuu ni kweli tunatakiwa kuwa na uelewa japo kidogo wa vitu tunavyokula na sehemu zenyewe za kupata huo uelewa ni pamoja na humu tunapo badilishana uelewa, lakini kwa style yako sijui kama kuna msaada hapo. Nadhani maelekezo yako yalitakiwa yaelezee kama yanafaa ni kwanini!? Na kama hayafai ni kwanini!? Fullstop! Hoja ya kuanza kujiuliza sijui uanaongeza kilo ngapi, yana kiasi gani sijui cha nini na nini, majibu hayo hayaji kwa kujiuliza tu!! Bali hutoka kwenye vyanzo vya maarifa ambapo kama unafaham unasema kama hujui unacoool tu!