Hao ni wanawake wa kiswahili.kiasilia m/mke anatakiwa kutunzwa na kujaliwa na mumewe hata kama ana hela kiasi gani itabidi tu uwe unampatia vizawadi ili aone unamjali hata kama ana kipato zaidi unaweza kumwomba hela kisha unamnunulia zawadi kwa hela yake hiyo hiyo ili mradi ajue kuwa unamjali
hivi katika maisha ya sasa ambapo unakuta mwanaume ameoa mke mwenye kipato eg. mhasibu, mhandisi, au ambaye ana shughuli zake binafsi za kumwingizia pesa ya kutosha kwa wao kama mke na mume kushare majukumu ya kuendesha familia mfano watu siku hizi wanashare ujenzi,rent,bill za nyumbani,ada za watoto et.., je ni sahihi kwa manaumwe kumpa mkewe pesa za matumizi yake binafsi? pesa kwa ajili ya mke kununua mavazi,kwenda saluni nk nk! au hii kwa sasa dhana iliyopitwa na wakati na ya kiutamaduni zaidi?? au kwa kuwa mke anauwezo wa kupata kipato haina sababu kwa mwanaume kumpa mkewe fedha za matumizi?
kwenu wadadavuzi naomba kuwasilisha!
kwa kweli.....vitu vingine ndo maana wanaume wakienda nje...ukimuuliza anasema we shida yako nini??kwenda kwangu nje kuna ulichokosa,hela si unapata,kodi unalipa wewe.gari umenunua wewe......kama huwezi waweza enda......heeeeeee.....uomba omba mwingine siyo......:decision::decision:
Mwanamke aliyeolewa anahitaji security toka kwa mumewe. Upendo wa mume kwa mke ni moja ya vitu ambavyoonyesha mwnamke yuko salama kwa mumewe. Kumpa pesa za vitu kama saloon ni muhimu sana kwani huonyesha upendo wa mume kwa mke. Mwanamke ni mwanamke tu! haijarishi anapesa kiasi gani.
Nailyine unakuwa kama huwajui wanawake bana? dem wa kiswahili chake ni chake hata kama ana mamilioni na cha mme/bwana/hawara ni chenu wote hata kama ni ndururu!
yani NI SAHIHI KABISA KABISA....hata kama nna kipato ...NKIOMBA NAULI NIPE,HELEA YA NGUO NIPE...WANAUME WAMEUMBWA MATESO.....nafikiri ni sahihi wtaoe na mi napewaga..japo mtu analalamika lakini ndo hivyo si wanawake tunamabo mengi wao hilo tuu aaaha.....YANI ATOE KWA MOYO 1....HATA KAMA NIMEMZIDI MSHAHARA....and i love this part.......anavyolalamika pale....lol...:wink2:
yani NI SAHIHI KABISA KABISA....hata kama nna kipato ...NKIOMBA NAULI NIPE,HELEA YA NGUO NIPE...WANAUME WAMEUMBWA MATESO.....nafikiri ni sahihi wtaoe na mi napewaga..japo mtu analalamika lakini ndo hivyo si wanawake tunamabo mengi wao hilo tuu aaaha.....YANI ATOE KWA MOYO 1....HATA KAMA NIMEMZIDI MSHAHARA....and i love this part.......anavyolalamika pale....lol...:wink2:
kwa mtizamo wangu mwanamke anatakiwa ajirembe mwenyewe,kama nguo anunue mwenyewe ntamsaidia pale ntakapojisikia lakini isiwe ni lazima.Au ndio nyie mnaingia bar unamwachia mumeo afungue pochi yake hata kumpa ofa hutoi au kumnunulia nguo mumeo apendeze huwezi.Kipimo cha mwanaume cha kumpata mke mwema ni yule anaeijtoa kwa wajili yako sasa siku sina kazi atanistahi kweli?CHa kushangaza unakuta ana mshahara mzuri lakni hata kuchangia ujenzi au ununuzi wa kiwanja hataki,anataka kuvaa nguo za gharama na magold wkt huo huo mnakaa nyumba ya kupanga ni ajabu sana.Wanawake badilikeni sasa wanaume watunzeni kama watoto wenu, hata mke ambae hana kazi lakini kwa mwerevu atajitahidi kusave hela anayopewa ya matumizi na kumsuprise mumewe kwa zawadi..
ndiyo ni haki yake kabisa kumuhudumia vitu kama mavazi salon na mengine pia kazi yake isyo sababu ya ww kutokumuhudumia huyo ni mkeo ni jukumu lako kumtunza,umeuliza swali zuri sana hope litachangiwa vilivyo mana mnajisahau sana mnapokutana na mwanamke mwenye kazi sometime hata hayo ya msingi hamyafanyi unamuachia kila kitu.
Umegusia kitu cha muhimu sana. Kama huyu mwanamke ana kazi yake inayompatia mshahara mzuri tu na bado tena hata hela ya saluni anategemea kwa mumewe na pengine mumewe ana kipato cha kawaida, mimi naona huo kama ni ubinafsi. Na mara nyingi hili jambo limeleta kutoelewana zaidi hasa kwa upande wa ndugu wa mwanaume. Mfano, unakuta mshahara wa mwanamke kazi yake ni kusaidia upande wa kwake (ndugu zake na kuendeleza kwako), kwa hali kama hiyo upande wa mwanaume mara nyingi inakuwa ni issue kuendeleza/kusaidia upande wa ndugu zake, sababu kubwa ni kuwa hela inayopatikana inakuwa haitoshi (inatumika mpaka kufanya vitu vingine ambavyo hata mkewe anaweza kuvimudu mfano wa hili la salun). Ikiwa tu mwanamke mpaka kiasi kidogo cha hela ya saloon anakomaa umpe (na ukizingatia ana mshahara wake) basi sidhani kwa mwanamke kama huyo atakuelewa incase umwambie mchangie suala la kodi, ada, etc. Lakini mwisho wa siku kinachohitajika ni maelewano jinsi ya kujipanga kwa suala zima la huduma kwa ujumla, lakini pia sio vibaya kwa siku moja moja kwa mwanaume kumpatia hela ya saluni mkewe bila kujali kama ana mshahara wake kwani hii inaongeza upendo na hali ya kujali zaidi.sasa na zile anazopata zinaenda wapi kama kila kitu uhudumie mwanaume?