Investa investa investa hivi kwa nini wasiondoke na hizo sehemu wakabidhiwe wazawa waone tutakavochapa kazi.What is investa by the way if they are coming all the way from wherever they are coming without any capital na wanapata capital hapahapa na zaidi wanaondoka pia na faida.Mimi kwa upande wangu I really hate the so called investa maana kwa kifupi wanatuuibia tu basi, bora waione ni nchi isiyo salama bhaaaaaaaaasi
Mpendwa hii ni case mistaken identity. Uongozi uliowapokea investors hapa Tanzania umewafanya watambuliwe vibaya na jamii. Wewe ni miongoni mwa wengi wanaowaona investor kama tatizo, lakini hii ni kutokana na vile walivyoingizwa, walivyotambulishwa na kutambulika katika mazingira waliyoyakuta hapa.
Canada na Uingereza vinajengwa na Wahindi; haohao investors ambao wewe unasema huwataki. Afrika ya Kusini imejengwa na investors kutoka sehemu mbalimbali kama vile Marekani, Uingereza au hata Israel, kama taarifa nilizo nazo ni sahihi.
Investors wakitumiwa vizuri wanaongeza ajira katika nchi, wanaingiza teknolojia mpya katika nchi, wanakuza kipato cha Taifa, lakini unahitaji serikali makini kuwaingiza, kuwaongoza, kuwalinda na kuwatawala. Ukiwa na serikali dhaifu, serikali manipulable, serikali yenye watu wenye IQ za kuku linazuka tatizo.
Soma Historia ya Visiwa vya Hawaii ndipo utatambua kuwa huwa kunakuwapo upande wa kisiasa wa Investors ambao unahitaji serikali makini kunusuru interest za taifa. La sivyo Investors wanaweza kuwa tatizo hata la kusababisha kupoteza utaifa.
Kwa hiyo nilitaka nisema usihukumu investors kama watu wabaya kihivyo kwa sababu kiuchumi ni watu wazuri. Chunguza umakini wa SErikali yako kuona kama wanao uwezo wa kufanya investors wawe tija kwa taifa kama ilivyo katika nchi nilizozitaja. So tatizo linaweza kuwa wewe na serikali yako na siyo investors !