Ni sawa kufunga ndoa na mwenye jina sawa na mzazi wako

Najijua

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
1,040
Reaction score
182
wadau naweka hoja ya haja jamvini, je ni sawa kuoa/kuolewa na mtu mwenye jina sawa na mzazi wako?
 
Great Thinker at work..............................

Umefika mbali kweli ndugu unaanza na jina tena??? Ukabila, udini, utaifa nk sasa na jina tena kisa linafanana na mzazi inahusu nini hasa kwa hapo???...................................oa/olewa tu maana mpaka umefikia hatua ya kutaka kuoa/kuolewa mlianzia mbali sasa iweje leo???
 
kwani unaoa/kuolewa na jina au mtu mwenyewe??
 
haina uhusiano kabisa hii we endelea na process tu
 
Jina lina matter muda fulani kwa kuwa mkiwa hata kwenye kupeana raha kuna kuitana majina mfano "asante ... Juma/Asha Baba/Mama" huoni unaweza kuwa unataja mzazi wako?

Kwenye kurithisha majina watoto, mtoto si sawa akawa na jina la mama/baba then ni sawa na babu na bibi yake, kwa wazungu ndio wanaleta majina ya Junior but ki afrika hatuna utamaduni huo kabisa

naweka hoja ya haja
 
Ni poa tu,lakini wakati wa malavidavi lifupishe.
 

Hiyo bold imenichekesha sasa hoja ni ipi?? Kama unaona jina unaita mzazi wako achana nae tafuta wa jina tofauti shida iko wapi sasa bana na wewe kha!!!!!!!!!!!!!!
 
wadau naweka hoja ya haja jamvini, je ni sawa kuoa/kuolewa na mtu mwenye jina sawa na mzazi wako?








Hio hoja yako ingeambatana na mawazo, walau tungeelewewa where its coming from...
 
Tumia akili kukataza mawazo shenzi kama haya .....ungekuwa karibu ni kwenzi ndo nakupa jibu...
 
hahahahahahahhhhaah mhh jina lina nini sasa,na hata mambo ya kuwapa watoto majina ya wanafamilia yamepitwa na wakati....chonde msinitoe macho wenye watoto wenye majina mpaka ya jirani zenu!
 
Jaman tuwe tunatabia ya kukaa chini kwanza na kuanza kufikiria kabla ya kuuliza! Sasa kinachotawala katika ndoa ni majina au Upendo jamani.. Isije ikawa jf ndo jalala la ushauri mambo mengine hata mtoto anaweza kukushauri..
 
Lengo sio kuwa kwaza wenye wake au waume wenye majina ya wazazi wenu ni kuuliza tu jamani
 

samahani kaka/dada...huna hoja ya haja kabisa.
 
What is wrong with it? Do you love a person or a name? ask yourself those questions and you will get an answer!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…