Faida za uvaaji wa condom wakati wa tendo la ndoa ni nyingi ikiwemo; ni njia ya uzazi wa mpango, kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa maji maji ya mwili. Nikirejea swali lako, ukishiriki mapenzi kwa njia ya mdomo (kunyonyana) kuna hatari (risk) ya kuambukizwa baadhi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo Herpes, Hepatitis B, Hepatitis C, HPV, HIV na mengine ikiwemo risk ya saratani ya koo (kutegemeana na factors nyingine nyingi). Kwahiyo faida ya kutumia Condom baada ya kushiriki mapenzi kwa njia ya mdomo ni utazuia mimba.