Pre GE2025 Ni sawa kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuandika barua kwa niaba ya CCM? Je, anaweza kuandika kwa niaba ya CHADEMA au ACT pia?

Pre GE2025 Ni sawa kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuandika barua kwa niaba ya CCM? Je, anaweza kuandika kwa niaba ya CHADEMA au ACT pia?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Jana tar 6/7/2024 CCM walikuwa wanazindua Kampeni kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ushiriki wa Vijana katika Chaguzi hizo katika Uwanja wa Mkapa, ambapo ilihitaji ushiriki wa wanafunzi pia ili kukamilisha tukio hilo.

Shughuli ni za kichama, ambapo waliotakiwa wakodi magari hayo ni chama wenyewe na siyo serikali.

Hiyo ni shughuli ya kichama ambayo haitakiwi kutumia rasilimali za umma kufanikisha shughuli zao wala serikali kuhusika kwenye kuandaa barua zao ili kufanikisha shughuli ya chama. Kwenye hili CCM ilitakiwa kuandika barua kuomba magari kutoka kwenye shule hizo wao wenyewe. Kitendo cha serikali kuandika barua hiyo kuomba magari hayo kwa shughuli za chama ni sawa na kusema sasa chama na serikali ni kitu kimoja.

Aliyesaini barua hii amesaini kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, akiandika barua kwa kuomba magari kutoka kwenye shule binafsi ili katika shughuli za chama. Wakurugenzi pamoja na maafisi wengine wa serikali ni watumishi wa umma ambao hawatakiwi kujihusisha na shughuli za kisiasa, akitaka kufanya hivyo inabidi aache kazi aende kwenye shughuli za kisiasa kwa tani yake.

1720340703726.png

Moja ya majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni Kusajili vyama vya siasa na kuvifuta vile ambavyo vimekiuka masharti ya usajili kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya mwaka 1992, lakini sheria hii ni kama imetungwa kwaajili ya upinzani, sijawahi ona CCM ikikemewa hata mara moja licha ya kwenda kinyume na sheria mara kadhaa!

Msajili na Ofisi yako mnajua majuku yenu kweli? Hata kama ndio CCM yaani mnafanya ujinga mpaka inakuwa too much! Nyinyi kama wasimamizi wa sheria mnatiwa kuwa mfano, lakini ndio kwanza mnaongoza kwa upuuzi, mnategemea wananchi wajifunze nini kutoka kwenu?

1720340265746.png

Si mara ya kwanza CCM kufanya hivi, ni makusudi kabisa kwanini Msajili wa Vyama unaangalia ukiukwaji huu wa wazi wazi wa sheria? Majuzi Waziri Mkuu Majaliwa alifanya mkutano na wananchi jimboni kwake akiwa amevalia sare za CCM nako wala halikukemewa.

Pia soma: Kwanini CCM mnafanya kampeni wazi wazi wakati muda wa kampeni bado? Msajili wa Vyama vya Siasa hulioni hili?

Tupigie tu mstari sasa msajili wa vyama anatakiwa kuwa CCM ili kufanikisha mipango ya chama, maana upo tu, unachojua ni kuhenyesha wapinzani wakiharibu na wakati mwingine ni kwa uonevu ila CCM aaah.

ccm.jpg

YAH: OMBI LA GARI/MAGARI KWA AJILI YA SHUGHULI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI UWANJA WA BENJAMINI MKAPA

Husik ana mada tajwa hapo juu.

2. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam inaomba magari kwaajili ya shughuli za Chama Cha Mapinduzi zitakazofanyika katika uwanja wa Benjamini William Mkapa.

3. Shusghuli hizo zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 06/07/2024 ambapo magari yanatakiwa kukutana katika Chuo cha Ustawi wa Jamii – Mwenge saa moja asubuhi.

Wewe ukiwa mmojawapo wa wadau wa Elimu wa Manispaa hii unaombwa gari/magari kwaajili ya kazi hii muhimu.

4. Tafadhali posho ya dereva na mafuta vitapatikana.

Asante kwa ushirikiano.

Imesainiwa
Deograsia A. Mapunda

Kny; MKURUGENZI WA MANISPAA

Nakala: Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni – Aione kwenye jalada
 
Sasa omba wewe kutoka huko chamani kwenu uone mabavu ya msajili. CCM is HIV in the Tanzanian political body..
 
Naona barua imeandikwa na mkurugenzi. Ilikuwa ni shughuli gani mkuu? kama ni ya kiserikali na haikuhusisha wanafunzi bali magari tu pengine sio shida. Kama ni za kisiasa itakuwa shida na ikahusisha wanafunzi.
Tumia akili kabla ya kuchangia. Gari kila linapotumika kuna depreciation expenses. Magari ya kukodi yako mengi.
 
Back
Top Bottom