Ni sawa mwanafunzi kamaliza form 6 hajui hata kuandika "hello world" ila anategemea kusomea computer science / engineering kutamfanya awe nondo ?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Maeneo ya kazini huwa kuna madogo wa chuoni hapa nafahamiana nao wakiniletea kazi za viti, vitanda, meza, n.k.

Sasa mwezi uliopita kwenye pirika pirika za vyuo kufungua katika story za hapa na pale kuna madogo walikuwa wanapiga story za ku code, kuna mwenzao alikuwa kamaliza certificate kaingia diploma anawaambia hawajui chochote kuhusu ku code ila wale wenzake wa six wanaoingia degree wanamwambia yeye hajajifunza chemistry ya form six kwa hio kuna vitu hajui.

Mimi nikaingiza maada ndogo tu, nikawauliza wale wa six, mnajua kuandika hello world kwa lugha yoyote, wakadhani labda ni kichina ama kiarabu, mwenzao yule mwengine nae anawapa pressure wajibu ila hawakuweza kujibu.

Nilibaki nashangaa sana inakuwa vipi mtu anaingia degree hawezi kuandika hello world kwa lugha yoyote.

Sisemi kwamba hawawezi kujifinza kwa kuchelewa but come on guys! Mtu hujawai weka effort yoyote japo hata kujua basics za kitu unaenda somea degree 😳 ni kama vile unaenda kujifunza kufua nguo zako sekondari boarding
 
Maeneo ya kazini huwa kuna madogo wa chuoni hapa nafahamiana nao wakiniletea kazi za viti, vitanda, meza, n.k.

Sasa mwezi uliopita kwenye pirika pirika za vyuo kufungua katika story za hapa na pale kuna madogo walikuwa wanapiga story za ku code, kuna mwenzao alikuwa kamaliza certificate kaingia diploma anawaambia hawajui chochote kuhusu ku code ila wale wenzake wa six wanaoingia degree wanamwambia yeye hajajifunza chemistry ya form six kwa hio kuna vitu hajui.

Mimi nikaingiza maada ndogo tu, nikawauliza wale wa six, mnajua kuandika hello world kwa lugha yoyote, wakadhani labda ni kichina ama kiarabu, mwenzao yule mwengine nae anawapa pressure wajibu ila hawakuweza kujibu.

Nilibaki nashangaa sana inakuwa vipi mtu anaingia degree hawezi kuandika hello world kwa lugha yoyote.
Mimi nilihitimu form VI sikuwa najua hata mouse ni nini!.

Lakini nikaenda kuchukua shahada ya sayansi katika elimu na computer!.

Mbona kwenye TCU guidebook hakuna hivyo vigezo vya lazima uwe na computer knowledge ndio uchukue shahada ya ICT, Computer Sciences or Computer engineering!.

Usiwatishe!.
 
Naungana na wewe mkono sio lazima ujue ndio uende ukasome mambo ya kucode.

wanaweza jifunza watakapofika chuo wakiwa na bidii na wakawapita wanaosoma degree. naungana na wewe kabisa. tuwatie moyo
 
Watu wanakua programmer hata baada ya kumaliza degree zengine na kufanya kazi miaka mingi career tofauti kabisa, kuna manesi, accountants, waendesha malori wote hawana experience yoyote ya programming lakini wamebadili careers kuwa programmers. Ni advantage kuanza mapema ila sio lazima.
 
Mi nlienda chuo hata computer sijawahi gusa. Hao waliotoka diploma wanajua vitu kidogo baadae walikuja kuomba msaada kwenye kucode.
 
Kwahyo kujua kuandika
'hello world'

Unakuwa umegraduate programming eti?

There's so much to it..
Mimi nikajua umetumia hata 1% ya ubongo wako kushauri mitaala yetu iingize rasmi hizi course kwenye mashule yetu kuanzia primary mpka secondary
Unaleta huu utopolo
 
Mtoa mada nimekuelewa vizuri.

Apart from hao wa A level, kuna watu wa Degree kabisa ukimfichia desa hapo mwambie achape code bila kukosea syntax hawezi. Atababaika mnoo.

Mie mwanangu akiwa na miaka 8 tyr Html,CSS na PHP iwe imelala kichwani.. akifika 10 yrs namleta kwenye Cyber security courses na mimi mwenyewe namfunda labda Mungu awahi kuniita.
 
Hakuna tatizo, mimi sikujua siyo tu Hello World hata Computer sikuwahi kuigusa achilia mbali kuiona ila sasa hivi naweza kuprogramm C/C++, fortran au hata python.

Kumbuka siku zote siyo swala la access bali ni uwezo wa kujifunza ndiyo kitu muhimu, …
 
Mtoa mada nimekuelewa vizuri.

Apart from hao wa A level, kuna watu wa Degree kabisa ukimfichia desa hapo mwambie achape code bila kukosea syntax hawezi. Atababaika mnoo.

Mie mwanangu akiwa na miaka 8 tyr Html,CSS na PHP iwe imelala kichwani.. akifika 10 yrs namleta kwenye Cyber security courses na mimi mwenyewe namfunda labda Mungu awahi kuniita.
Ahsante mkuu kwa kuwa na wazo kama langu mimi wa kwangu kamaliza form four mwaka jana na anatarajia kwenda advance ila mpka sasa anaunda website vizuri bila shida na kuna shule kaitengenezea school management system mwanzo mwisho ni vitu vichache sana aliuliza kwa mwalimu wake
 
Back
Top Bottom