Ni serikali iliyofeli au wanafunzi?

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,129
Ebu pitia hIki kinachoitwa “vision”, mission” na sehemu ya katiba yetu.

MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATINAL TRAINING

VISION
To have a Tanzanian who is well educated, knowledgeable, skilled, and culturally mature to handle national and international challenges in various political, and social-economic fields by 2025.

MISSION
To ensure that there is an appropriate legal and practical working environment to enable all stakeholders who are eager and able to provide quality education participate in its expansion at all levels and provide equal opportunities to all; as well as enhancing cultural administration, supervision and infrastructure.

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977
11(2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.

11(3) serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule ma vyuo vinginevyo vya mafunzo,

Katika matokeo ya mwaka 2010, ilidaiwa kwamba wanafunzi zaidi ya nusu walifeli (wameshindwa kupata alama mbili za D). mimi sikushtushwa na haya matokeo sababu niliyategemea kutokana na mchakato wa zinazoitwa shule hasa za kata zinavyoendeshwa.

Ifahamike kwamba shule ni mchakato unaoendelea kati ya mwalimu na mwanafunzi hivyo uwepo wa majengo pamoja na wanafunzi pekee hakukamilishi maana ya shule. Je hapa asiyekuwepo shuleni anafeli vipi? Watoto wanafeli vipi wasichofundishwa? Hivi somo lenye mada 40, alafu mwanafunzi akafundishwa mada 3, hapa tunategemea mtoto atumie miujiza gani ili afaulu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…