Ni serikali tatu,sio mbili na wala sio moja:

MMASSY

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
290
Reaction score
196
Mwendelezo wa Uchambuzi wa Rasimu ya Katiba.
SEHEMU YA SITA

MUUNDO WA SERIKALI YA MUUNGANO
Ibara ya 57(1a-c) na (2a-c).Inazungumzia kuwa Tanzania kutakuwa na serikali tatu(3)yaani ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania Bara.Hili ni wazo zuri sana na kwa kuwa haya ni maoni ya wananchi wengi na tangia siki nyingi,ni vizuri kifungu hiki kikabaki kama kilivyo kwa kuwa ndio njia sahihi na pekee ya kuendelea kuwa na Muungano hasa kwa mazingira haya ya utandawazi.Ni kwanini tuwe na serikali tatu?
i. Uhuru zaidi kwa serikali za Tanganyika na Zanzibar.Kumekuwa na msuguano wa kimaneno na hata mara nyingine kuibuka nguvu katika suala la kutetea ZANZIBAR kuwa na mamlaka kamili na yote haya yalitokea Zanzibar kwa idadi ya wananchi kutaka kuwa na serikali yao yenye mamlaka.Kuwa na serikali za Tanganyika na ile ya Zanzibar kutawezesha serikali husika kufanya mambo yake kwa uhuru zaidi isipokuwa maswala yale ya Muungano ambayo pia yameainishwa katika Rasimu hii.Kwa kuwa kila upande utakuwa na serikali yake,Mahakama zake na hata Bunge lake,itawezesha nchi husika kuweza kuendesha mambo yake kwa uhuru zaidi na kuyaacha yale yaliyo ya Muungano tu ndio yashughulikiwe na mawaziri wa Muungano.Hili limefanyika katika nchi za wetu kama Marekani na Muungano wao umedumu bila manung’uniko kwa miongo kadhaa nab ado upo imara.
ii. Usimamiaji mzuri na mgawanyo wa Rasilimali za umma.Kwa sasa kuna maswala yanayogombaniwa japo kwa maneno katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na rasilimali za taifa.Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wamesikika wakilalamika kwamba wananyonywa katika ugawaji wa keki ya taifa,kuna pia baadhi ya maswala kama Gesi na mafuta yana mvutano kama yawe ya Muungano au la.Katika mazingira na kwa kuwa kila upande utakuwa unasimamia rasilimali zake,ni vyema sasa kwa Rasimu hii kutokanusha uwepo wa serikali hizi tatu ili kutoa fursa kwa kila upande katika Muungano kusimamia ipasavyo rasilimali zao na kuwaletea wananchi maendeleo na kuyaacha tu yale ya Muungano ndiyo yashughulikiwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
iii.Kuna hoja zinatolewa pia kuwa kuwa na serikali tatu ni gharama kuziendesha.Kitu ambacho wakosoaji wanshindwa kukianisiha mpaka sasa ni gharama halisi zitakuwa za kuendesha serikali hizo.Wameshindwa kueleza namna serikali hizi zitakuwa na gharama kuziendesha kwa kuwa kuna ukweli kwamba kuwa na serikali ghali ama nafuu inategemea katiba yenyewe inavyosimamia rasilimali za wananchi na namna inavyowabana viongozi waandamizi wa hizi serikali kutokuwa wabadhirifu na kuendesha serikali kwa anasa.Kwa sasa taifa linasumbuliwa na gharama kubwa za uendeshaji wa serikali japo tuna serikali moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ndogo ya Zanzibar.Kwa nchi za wenzetu kama ile ya Marekani inayoongozwa na majimbo makubwa kuliko hata Tanzania 53,kila jimbo linajiendesha lenyewe isipokuwa tu kuna serikali ya Shirikisho(Federal Government anayoongoza Barack Obama ambayo kwa mujibu wa katiba ya Marekani Ibara ya 1(8) inaiwekea serikali ya shirikisho mipaka mikali ya utendaji wa serikali katika matumizi ya fedha za umma katika maswala kama vile Ulinzi wa taifa,mfumo wa mahakama,ujenzi wa barabara,ofisi za posta na kulipa kodi ya taifa.Wenzetu wameiwekea serikali ya Shirikisho mipaka ya matumizi ya fedha ili kuacha mwanya kwa serikali za majimbo 53 uhuru wa kusimamia vizuri maendeleo yao.Hili limefanikiwa sana katika historia ya taifa la marekani kwa kuwa wao hawakutazama uendeshaji wa serikali kama ni gharama kubwa kwa sheriamadhubuti walizojiwekea bali walitazama gharama za kulinda muungano.Sisi pia tunaweza kuzuia matumizi makubwa ya serikali hizi kwa kuziwekea mipaka ya madaraka na matumizi ya fedha za walipa kodi.Kuendesha serikali kwa gharama kubwa ama ndogo ni utamaduni tu ambao umezoeleka na tunaweza kama Watanzania kuukataa na fedha au rasilimali nyinginezo za nchi zikatumika kwa maendeleo ya wananchi.
iv. Umoja na ushirikiano;ni ukweli usiopingika kuwa hata wanaopinga serikali tatu wanatambua kwa mazingira ya sasa kuna kundi moja linanyimwa haki zake ama la Zanzibara ama la Tanganyika.Hii ni kwa kuwa unapokuwa na serikali ya Zanzibar na ile ya Jamhuri manake ni kwamba hawa Watanganyika wao hawana serikali ama unaitumia hii serikali ya Jamhuri ya Muungano kama serikali ya Tanganyika kitu ambacho pia kitakuwa si haki kwa Wazanzibari.Kimsingi kwa mfumo ulipo sasa ni kwamba serikali ya Jamhuri inafanya majukumu ya Muungano na yale ya Zanzibar kitu ambacho kimejengea watu wa Zanzibar taswira kwamba wanaamuliwa mambo yao na watu wa Tanganyika(Wabara).Kwa mazingira haya,tunapaswa kuwa na serikali tatu kama rasimu inavyopendekeza ili kuwe na serikali mbili za pande zote mbili za muungano na serikali moja kuu ya Muungano ambayo itakuwa ndiyo serikali kuu(mama).Likipitishwa hili basi tutakuwa na Muungano imara kuliko sasa kwa kuwa kila upande utakuwa na serikali yake lakini kuna serikali moja kuu ambayo itapatanisha pia serikali za washirika pale wakigombana.Kwa muundo wa sasa ukitokea ugomvi kati ya Zanzibar na Bara ni ngumu kuumaliza kwa kuwa kuna mlalamikaji mmoja ambaye ni Zanzibar halafu kuna mwamuzi na mlalamikiwa ambaye ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Tumeona siku zote Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kimsingi inahusika kutatua kero za muungano,miaka mingi imeshindwa kutatua na kumaliza kero za muungano kutokana na aina ya muungano tulionao.
MMASSY JEROME
0786141643

 
Soma post yote jangakuu usisababishe majanga
 
Naomba ubainishe kwa nini tusiwe na serikali moja?
Namuunga mkono MMASSY suluhisho hapa ni Serikali 3
Ukiangalia upande wa Zanzibar wao hata hiyo 1- hawataki 2- hawataki, 3- hawataki wao wanataka ya kwao tu
Sasa kuuendekeza Muungano bado ni mzigo mkubwa,
Kuwa na Serikali 3 itasaidia kuona kila Serikali inasimamaje na baada ya muda ndio tutapata jibu au tuuvunje Muungano au tuujenge urudi kwenye Serikali 1
Kwa CCM kulizungumzia hili ni kuogopa kivuli chake kwani G-55 walishatanabaisha turudi katika Tanganyika yetu
 
Last edited by a moderator:

ni kweli kabisa Kaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…