Ilikuwa jana majira ya jioni,moto ulionekana kuunguza mbuga katika eneo la Jeshi Kikosi cha Ihare nyuma ya Uwanja wa Ndege Jijini Mwanza. Abiria tulishushwa ndani ya Bus na Askari wa Jeshi la Wananchi kwenda kuzima moto. Abiria tuliitikia amri hiyo tukazima moto na kupanda Bus letu. Wakati sasa Dreva anataka kuondoa gari,maskini alikuja kijana mwendesha Boda boda ambaye nina amini hakujua kilichokuwa kinaendelea akapita. Kijana huyo alifatwa kwa kukimbizwa na Pikipiki alikutwa njiani alipigwa sana na Askari hao ambao kwa utaratibu uliopo wanajulikana ni akina nani waliokuwa kwenye zamu jana jioni. Tabia hii haijaanza jana, wapo watu wengi ambao walishakutwa na mkasa kama uliompata mwendesha Boda boda,kwa kupigwa na kuadhibiwa kijeshi. Sheria inasemaje kuhusu tabia hii na nini kifanyike kukomesha tabia hii?